Avuae Nguo Huchutama.

Grace Mshanga - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Grace Mshanga (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Neno avuae ni kisifa kinachotokana na tendo la kuvua nguo. Msemo huu unamaanisha avuae ni tendo la kuvua nguo na kubaki utupu. Kuchutama ni kuinama kwa ajili ya kuficha utupu.

Mwanadamu ana asili ya kuona aibu, hivyo akitoa nguo ni lazima achutame ili afiche utupu wake asionekane na mtu.
Maneno haya yanaweza kufananishwa na mtu aikoseaye adabu jamii na halafu akaona aibu. Baada ya kuona aibu akakiri moyoni mwake kuwa alichokifanya si cha kiungwana bali kilimtia aibu katika jamii yake. Akiwa na busara humuomba Mungu amsaidie ili asirudie tena kutenda kosa kama lile.

Baada ya hapo huanza kutenda matendo mema na hujisahihisha ili asirudie tena.
Mambo ya aibu huweza tokea katika jamii, lakini pale unapokuwa umekosesa, yakupasa usafishe dhamira yako ili usirudie kuikosea tena jamii yako. Jamii ni yako na ni maisha yako. Huwezi kuishi bila jamii. Zingatia hilo.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Nazi Haishindani Na Jiwe!

Next
Next

Akiba Haiozi