Mpanda Hovyo Hula Hovyo.

Simulizi
by Grace Mshanga (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Neno mpanda linatokana na neno kupanda. Mpanda ovyo ni yule mtu anayepanda vibaya bila mpangilio. Mtu huyu hupanda bila kufuata hatua zitakiwazo. Mathalani, wakati wa kupanda inatakiwa kuzingatia nafasi kati ya mbegu na mbegu, hali kadhalika, kati ya mstari hadi mstari. Pia inabidi kuzingatia ubora wa mbegu zenyewe ili kupata mavuno yaliyo mengi na bora. La sivyo, kinyume na hapo, mavuno yatakuwa kidogo na yenye ubora duni. Pale mavuno yanapokuwa duni hayatakidhi kuliwa kwa mwaka mzima uliotegewa. Ndio maana ya usemi huu kuwa aliyepanda ovyo, atakula kwa miezi michache tu, kinyume na mategemeo yake.
Hapa tunajifunza mambo mengi. Hata watu wanapokuwa kazini wanatakiwa wafanye kazi kwa bidii. Kazi zao zinatakiwa ziwe na tija. Kila mfanyakazi anatakiwa awe na mpangilio mzuri wa kazi zake.
Kuna watu wana tabia ya kufika ofisini na kuanza kuchati kwenye makundi sogozi. Huweza kutumia hata masaa mengi bila ya kujali kuwa wako kazini. Wakati mwingine hufanya mambo ambayo
hayana msingi wowote kwa maendeleo ya mashirika yao. Si ajabu kuwasikia wakizungumza na kupashana habari zisizokuwa na msingi wowote kwa kutumia masaa mengi. Wengine huthubutu hata kuacha kazi zao, na kwenda kunywa chai kwa masaa. Tabia kama hizo ni sawa na za mpanda ovyo na kula ovyo.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection