Mkia Ukatikapo Ng'ombe Huona Umuhimu Wake!

Simulizi
by Grace Mshanga (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Mkia wa ng'ombe ni wa muhimu sana maana ndio anaofukuza nao inzi na wadudu wengine watambao ambao ni hatarishi kwake. Ng’ombe huyu huwa hawezi kuona thamani wala umuhimu wa mkia wake mpaka ukatike. Pale wadudu watakapomtambaa atashindwa kuwafukuza kutokana na mkia wake kukatika.
Katika maisha yetu yatupasa tutambue na tuone umuhimu wa watu walio karibu nasi. Mara nyingi watu hawa hutusaidia kifedha, kimawazo, na hata jinsi ya kuishi na watu wengine pamoja na jamii inatotuzunguka. Tusiwe watu wa kuthamini na kutambua umuhimu wa mtu wakati ameshatangulia mbele za haki. Yatupasa tuwape sifa stahiki wakati watu hao wangali hai ili nao waweze kujisika kuwa unathamini yale mambo mazuri wanayokufamyia.
Hatutakiwi kumumwagia sifa sifa wakati amekwishaondoka hapa duniani kwani sifa hizo yeye hazisikii, bali zinakuwa ni za kuwafurahisha wale waliohudhuria mahali pale. Tujifunze kuwa waungwana kwa kuyaheshimu na kuyathamini yale tunayotendewa na binadamu wenzetu.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection





