Jembe Halimtupi Mkulima!

Grace Mshanga - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Grace Mshanga (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Jembe ni nyenzo inayotumika na mkulima wakati wa kilimo. Kuna majembe ya aina mbalimbali, mfano, jembe la mkono, jembe la kukokotwa na ng'ombe. Hali kadhalika, kuna majembe ya kufungwa na kukokotwa na trekta. Hii yote ni kumwezesha mkulima alime na kupata mazao ya kuridhisha ili aweze kujikimu.

Tunaposema "jembe halimtupi mkulima" tuna maana kubwa. Mkulima hata kama angelima mahali padogo kiasi gani ili mradi tu hali ya hewa ikawa nzuri, ana uhakika wa kuvuna. Pili tunaona kuwa mkulima sio mtu wa kukata tamaa, yeye hulima hata hali iwe ngumu kiasi gani, yeye hubaki kuwa ni mvumilivu na huwa yuko tayari kungojea mavuno.

Kwa uhakika, jembe halimtupi mkulima hivyo vijana mnaaswa mjiajiri kwenye kilimo. Baada ya muda mtakuwa watu tofauti ikilinganishwa na pale mwanzo. Mtakuwa na kipato cha kuridhisha, na hata pengine mkakidhi vigezo vya kuitwa matajiri.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Tunda Jema Halikai Mtini.

Next
Next

Mkia Ukatikapo Ng'ombe Huona Umuhimu Wake!