Njia Ya Mkato Tamu, Lakini Ina Madhara

Njia Ya Mkato Tamu, Lakini Ina Madhara

Mara nyingi kama mtu anataka afike haraka, anatafuta njia ya kukatisha, njia ya haraka. Njia hiyo inaweza kuwa nzuri pale tu utakapofanikiwa kufika kule uendako. Kuna wakati lakini njia ya mkato inaweza ikakupoteza na ukashindwa kufika uendako. Kuna baadhi ya binadamu, hupenda kutafuta mafanikio kwa kupitia njia ya udanganyifu, kama kutapeli wenzao. 

Read More
MTOTO WA MWENZIO NI WAKO

MTOTO WA MWENZIO NI WAKO

Kuna watu wenye uwezo mkubwa wa kusimamia shughuli na kuleta mafanikio makubwa katika jamii zao. Watu hawa huwa ni muhimili wa shughuli au kazi za mahali hapo. lnawezekana mtu mwenye kuzisimamia shughuli asiendelee kuwepo mahali pale kutokana na sababu mbalimbali, mathalani, magojwa, uhamisho na sababu zinginezo zikiwa ni pamoja na kifo.

Read More
Baba, Mama, Wote Tuwajibike

Baba, Mama, Wote Tuwajibike

Kuwajibika ipasavyo ni jambo la lazima kwa binadamu kwani usipowajibika kuna mahali hapatakaa sawa, yaani panaweza pakaharibika. Baba kama kiongozi wa familia anatakiwa kutimiza wajibu wake wa ubaba vile inavyotakiwa. Anapaswa kuiongoza, kuitunza, kuilinda na kuihudumia familia yake ambayo aliianzisha. Hii inatuambia kuwa, kuitwa baba siyo kuwa mwanaume suruali bali ni kuwajibika kwa kila hali kama mzazi.

Read More
Asiyekuwa Na Hili, Ana Lile

Asiyekuwa Na Hili, Ana Lile

Usemi huu unatufundisha kuwa binadamu tunatakiwa kuheshimiana katika kila hali. Hakuna sababu ya binadamu mmoja kujiona kuwa ni bora zaidi kuliko mwingine. Mungu alipomuumba mtu na viumbe vyote, alivipatia karama, kila kiumbe tofauti na ya mwingine. Ndio maana unakuta kila mtu ana taaluma yake tofauti na ya mwingine.

Read More
Utamu Wa Muwa Kifundo

Utamu Wa Muwa Kifundo

Miwa ni zao linalozalishwa kwa wingi ili kupata sukari. Viwanda mbalimbali nchini hufanya mchakato wa kupata miwa ili kutengeneza sukari. Mtu akitaka kula muwa ni lazima amenye maganda ili aweze kutafuna hiyo sehemu nyeupe ya ndani. Majimaji yenye utamu humezwa lakini makapi hutemwa. 

Read More