Usimkumbushe Mtu Mema Yako, Acha Dunia Imkumbushe
Kusaidiana katika maisha yetu ni jambo la kawaida. Hapa duniani tunategemeana. Hakuna aliyekamilika.
Hekima Ni Jambo La Msingi
Kile unachokiita baraka au ushindi kilianza kama tatizo. Mara nyingi, yule anayefanikiwa kutatua matatizo huonekana kama ana baraka au mshindi fulani hivi. Ni kawaida kwa kila mwanadamu kupata matatizo. Pale mtu anapopata matatizo, ni vema kutafuta mbinu za kupambana nayo. Wengi hujaribu kukimbia matatizo yanapotokea.
Ukishindwa Hili Leo, Kesho Utashinda Lile
Wakati sisi tunasoma shule ya msingi, ilikuwa ni madarasa manne tu, yaani la kwanza hadi la nne. Enzi hizo walizingatia sana umuhimu wa kila darasa kuwa na wanafunzi wasiozidi arobaini na tano.
Huwezi Kupanda Ngazi Ya Mafanikio Ukiwa Umeweka Mikono Mfukoni
Ni jukumu la binadamu wote kuwajibika katika maisha yetu ya kila siku. Huwezi ukafanikiwa bila kutoka jasho. Kufanya kazi kwa bidii, ndio siri kubwa ya mafanikio ya mwanadamu.
Kama Huwezi Kuwa Wa Msaada, Basi Usiwe Kizuizi
Watu wengi wamekuwa wakilalamika kila kukicha kuwa, maisha yanazidi kuwa magumu. Hali hiyo, imemlazimisha kila mtu kupambana kwa bidii ili mwisho wa siku aweze kupata kile alichodhamiria kupata.
MTOTO WA MWENZIO NI WAKO
Kuna watu wenye uwezo mkubwa wa kusimamia shughuli na kuleta mafanikio makubwa katika jamii zao. Watu hawa huwa ni muhimili wa shughuli au kazi za mahali hapo. lnawezekana mtu mwenye kuzisimamia shughuli asiendelee kuwepo mahali pale kutokana na sababu mbalimbali, mathalani, magojwa, uhamisho na sababu zinginezo zikiwa ni pamoja na kifo.
Maisha Yameficha Matukio/Mambo Usiyotarajia
Usemi huu unatufundisha namna tunavyotakiwa kuishi hapa duniani, siku hadi siku. Mambo ya jana sio ya leo, maana Mwenyezi Mungu ameiumba kila siku na habari zake mpya. Tupo hapa duniani na tunatakiwa kuishi kwa kutegemeana. Aliyekusaidia jana sio atakayekusaidia leo. Kila leo ina mambo yake tofauti.
Baba, Mama, Wote Tuwajibike
Kuwajibika ipasavyo ni jambo la lazima kwa binadamu kwani usipowajibika kuna mahali hapatakaa sawa, yaani panaweza pakaharibika. Baba kama kiongozi wa familia anatakiwa kutimiza wajibu wake wa ubaba vile inavyotakiwa. Anapaswa kuiongoza, kuitunza, kuilinda na kuihudumia familia yake ambayo aliianzisha. Hii inatuambia kuwa, kuitwa baba siyo kuwa mwanaume suruali bali ni kuwajibika kwa kila hali kama mzazi.
Asiyekuwa Na Hili, Ana Lile
Usemi huu unatufundisha kuwa binadamu tunatakiwa kuheshimiana katika kila hali. Hakuna sababu ya binadamu mmoja kujiona kuwa ni bora zaidi kuliko mwingine. Mungu alipomuumba mtu na viumbe vyote, alivipatia karama, kila kiumbe tofauti na ya mwingine. Ndio maana unakuta kila mtu ana taaluma yake tofauti na ya mwingine.
Aliyekula Vizuri Utamjua Wakati Wa Kunawa Mikono
Kama vile ambavyo binadamu hatufanani, ndivyo ilivyo katika maisha ya mwanadamu. Kuna watu ambao Mungu amewajalia kuishi maisha ya raha na ya kuridhisha. Lakini kuna wale ambao wanaishi kwa kutokuwa na uhakika wa maisha yao. Watu hawa hawaelewi pale wanapoamka, siku yao itapitaje. Vyovyote itakavyokuwa, kwao ni kwa kudra na neema zake Mungu.
Utamu Wa Muwa Kifundo
Miwa ni zao linalozalishwa kwa wingi ili kupata sukari. Viwanda mbalimbali nchini hufanya mchakato wa kupata miwa ili kutengeneza sukari. Mtu akitaka kula muwa ni lazima amenye maganda ili aweze kutafuna hiyo sehemu nyeupe ya ndani. Majimaji yenye utamu humezwa lakini makapi hutemwa.
Kuzaa Si Kazi, Kazi Kulea
Kila mtu anaweza kuzaa hata kama ana kasoro za aina yoyote. Kwa mfano, hata kichaa anayeokota makopo au matakata jalalani na kula, naye huwa anazaa. Ndivyo Mungu alivyotuumba. Kuzaa ni haki ya kila binadamu.
Unakosa Usingizi Kwa Ajili Ya Wanaokutegemea
Usemi huu unatulenga sisi wazazi au walezi. Mipango yetu na matumizi yanakinzana kutokana na majukumu yanayotukabili siku hadi siku. Ina maana mipango na mapato, hayo mambo mawili hayaoani. Mara nyingi, matumizi yanakuwa makubwa zaidi ukilinganisha na mapato tuliyonayo. Wengi wetu tuko katika eneo hilo.
Ukiona Neno, Usiposema Neno, Hupatikani Na Neno
Neno ni umoja linaweza kuwa na silabi hata kumi lakini linatambulisha kitu mfano "keti" ni neno la silabi nne, linatambulisha kitendo fulani kifanyike. Neno na neno likiunganishwa huleta maana nzuri zaidi mfano, “Eliza, keti karibu na babu". Hii sentensi inaeleza nani afanye nini na ni wapi.
Figa Moja Haliinjiki Chungu
Figa ni chuma au jiwe ambalo hutengenezwa kwa ajili ya kushikilia chungu au sufuria wakati wa kupika jikoni. Kimsingi figa moja au mawili hayawezi kushikilia sufuria jikoni kwa ufanisi kwani sufuria haitakaa vizuri au kwa uimara jikoni. Ili sufuria ikae kwa uimara jikoni, ni lazima mafiga yawe matatu.
Kila Changamoto Ni Somo, Na Kila Mpango Ni Hatua
Changamoto katika maisha ni lazima zimpate kila mtu anayeishi. Bila changamoto huwezi kusonga mbele ama kukamilisha malengo na mipango yako. Tukumbuke kuwa katika mipango tunayoitengeneza, ndio huwa mwanzo wa changamoto zake. Bila changamoto, huwezi kutekeleza yale uliyoyapanga. Hivyo basi, changamoto ni budi ziwepo.
Upendo Unaweza Kuwa Wa Kinafiki, Chuki Huwa Ni Halisi
Upendo ni neno ambalo huwa tunaliongelea siku zote katika maisha yetu. Mara nyingi, tunapoongelea suala hili, huwa tunakuwa na marafiki. Kwa kawaida, kuna marafiki ambao wanaweza kuwa ni wa karibu sana. Marafiki hawa huwa tuko huru nao na huweza kuelezana habari zetu hata pamoja na zile za ndani kabisa.
Ahadi Ni Deni
Deni ni kitu chochote ambacho umechukua kutoka kwa watu na unakuwa bado hujalipa. Deni linaweza kuwa ni pesa au kitu chochote ulichoazima kutoka kwa mtu huku ukiahidi kuwa utalipa ama kurudisha kwa wakati mliokubaliana.
Nimekupaka Wanja Wewe Umenipaka Pilipili
Wanja ni urembo mweusi unaopakwa na wanawake kwenye kope na nyusi kwa kwa ajili ya urembo. Pilipili ni tunda dogo linalotumika kama kiungo kwenye chakula. Pilipili ina sifa moja ya kuwasha sana. Ukiwa unakatakata pilipili, halafu ukaishika na kupeleka mkono wako machoni, adhabu utakayoipata hutakuja kuisahau. Hutaweza kulala mpaka upate dawa.
Wizi Wamsababishia Upofu
Upofu ni hali ya kupoteza uono. Vipo vyanzo mbali mbali vinavyosababisha upofu. Baadhi ya vyanzo hivyo ni pamoja na ajali, magonjwa ya kurithi na ya kuambukiza. Kuna wakati mwingine, chanzo kinaweza kutokana na tabia mbaya ya mtu, mathalani, wizi.