Machozi Ni Kiwakilishi Cha Hali Ya Uchungu Ama Furaha
Machozi ni yale maji yanayotoka kwenye macho. Maji hayo yanaweza kutoka Kwa ajili ya furaha ama uchungu. Kwa asilimia kubwa, huwa ni mambo ya uchungu. Machozi humwagika bila kifani pale mtu anapoondokewa na mpendwa wake. Kuondokewa na mtu, hasa yule wa karibu sana, mathalani, mtoto, mume, mke huwa ni uchungu mkubwa sana katika maisha ya mwanadamu.
Usimtendee Mwenzako Usiyopenda Kutendewa
Msemo huu una maana kubwa. Katika maisha, kuna kufurahi kwa aina nyingi, hasa pale watu wanapokutana, wakaongea na kutaniana. Kuna bwana mmoja alipenda sana kuwatania wenzake. Naye siku moja wenzie nao wakamtania yeye. Bila kujua, kumbe ule utani ulikuwa karibia na ukweli wa yale yanayotokea nyumbani kwake. Ulikuwa unamgusa barabara.
Ni Vizuri Kujua Kila Kitu Lakini Siyo Vizuri Kusema Kila Kitu
Kufahamu au kujua mambo ni utashi ambao Mungu amemjalia kila mwanadamu. Lakini katika kufahamu huko tunapaswa kuelewa mipaka ya ufahamu wetu na namna ya kukitumia hicho tunachofahamu.
Usikate Tamaa Kwa Kuwa Jua Limezama Wakati Nyota Na Mbalamwezi Hutoa Mwanga Pia
Usemi huu unatumika pale tunapokuwa tumekata tamaa baada ya kushindwa kwenye mipango tuliyokuwa nayo. Ni kawaida ya watu wengi kukata tamaa pale tunapokuta mambo hayaendi vile tunavyotarajia ama tulivyokuwa tumepanga.
Sio Sahihi Kila Mtu Kujua Changamoto Zako
Changamoto ni sehemu ya maisha kwa kila mwanadamu. Sote tunajua kuwa kila binadamu ana changamoto ambazo humfanya azihangaikie kutafuta ufumbuzi ama suluhisho lake.
Usiingilie Mazungumzo Ya Watu
Kuna watu katika maisha yao huwa wanapenda sana kuonekana wanaelewa sana habari nyingi za watu. Watu hao mara zote huwa wakiwakuta watu wako kwenye maongezi yao, lazima watajitahidi kuonyesha kuwa wanakijua hicho wanachoongea. Hapo hapo, huanza kuchangia bila hata ya kujua mazungumzo hayo yalianzia wapi. Tabia hii huwa siyo nzuri hata kidogo, inaweza kukuponza.
Hakuna Tajiri Anayemjali Maskini, Na Hakuna Maskini Anayemhurumia Tajiri
Mwenye uwezo mara zote huwa ana marafiki wengi ambao wana uwezo wa kulingana naye. Kutokana na uwezo wake, anakuwa hana muda wa kumjali maskini. Yeye huona kuwa matajiri wenzie wanaomzunguka wanamtosha kwa kila kitu. Wao ndio kila kitu kwake kwani akihitaji msaada ataupata bila matatizo.
Mchelea Mwana Kulia, Hulia Mwenyewe
Watoto ni zawadi kutoka kwa Mungu na wanahitaji msaada au uangalizi kutoka kwa wazazi/walezi, jamaa, ndugu, majirani, marafiki na jamii kwa ujumla. Watoto wetu mara nyingi hutenda makosa bila kujua au kukusudia, hivyo inabidi wanapokosea tuwakanye na kuwapa adhabu ndogo ndogo ili kuwaonyesha kuwa wamekosea.
Hakuna Siku Utakayomaliza Matatizo Yako Yote
Matatizo yameumbwa kwa kila binadamu aishiye hapa duniani. Pamoja na kwamba tunajitahidi kuweka mikakati ili kutekeleza mipango yetu, ni mara chache sana tutaweza kutimiza malengo tunayokuwa tumejipangia.
Mkopo Wasababisha Mama Akimbilie Mafichoni
Kukopa ni jambo la kawaida kwani hata serikali hukopa kwa malengo. Tatizo la kukopa ni pale mkopaji anaposhindwa kurejesha. Tumesikia visa vingi vinavyohusu mikopo lakini vingine vimeenda mbali na kumfanya mkopaji akimbilie mafichoni kusikojulikana.
Maisha Ni Kama Kuendesha Baiskeli, Usipokanyaga Pedeli Utaanguka
Maisha yanafananishwa na muendesha baiskeli. Maisha yanaendeshwa na nguvu zako mwenyewe, hakuna mafuta yanayotumika. Hivyo nguvu zako ndio mafuta yenyewe.
"Malezi Ruksa" Yana Athari Kwa Watoto
Malezi Ruksa (Permissive Parenting) ni aina mojawapo ya malezi ambayo mtoto anapewa ruksa ya kufanya au kuchagua chochote anachopenda/anachotaka bila ya kudhibitiwa. Malezi haya humpa mtoto uhuru uliopitiliza kiasi kwamba mtoto anasahau wajibu wake. Hata hivyo, hii ni aina ya malezi inayomfanya mzazi ajione anampenda sana mtoto wake.
KUWA MAKINI, CHUNGUZA USHAURI UNAOPEWA KABLA YA MAAMUZl
Gari ni aina ya chombo cha usafiri kinachoendeshwa kwa kutumia nishati ya mafuta na gesi. Dereva ndiye analiendesha na kulitunza gari. Endapo likipata hitilafu yeyote ile, dereva ndiye atakayelazimika kuteremka chini na kulikagua. Pale atakapogundua kama kuna hitilafu yoyote, ni wajibu wa dereva kutafuta mafundi wa kutatua tatizo hilo kwa kuwa wanayo maarifa ya kutosha.
Kuishi Kwingi Kuona Mengi
Kuishi ni neno linalotokana na maisha. Maisha ni siku au miaka tunayojaliwa na Muumba wetu baada ya kuzaliwa. Wenzetu wa zamani waliishi miaka mingi sana, wengine miaka 700 mpaka 900. Nyakati hizi tulizo nazo kuishi kwingi ni miaka 100 tu tena ni kwa wachache sana. Kuishi kwingi na kuona mengi hapa anazungumziwa mtu aliyeishi miaka 50 au 60.
Mafanikio Makubwa Yana Vikwazo
Njia nyepesi kabisa ya kutofika popote ni kusubiri ueleweke na kusifiwa na kila mtu kwa jambo uliloamua kulifanya. Uhalisia ni kwamba huwezi kueleweka kwa kila mtu na sio rahisi sana kusifiwa na kila mtu hasa jambo linapokuwa katika wazo ama hatua za awali.
Fuata Maadili Uishi Kwa Amani
Amani ni kitu cha msingi sana katika maisha. Unaweza kuwa na kila kitu katika maisha yako lakini ukikosa amani moyoni mwako, yote yanakuwa ni kazi bure.
Tuwapende Ama Tuwachukie Watu Kwa Kadri
Kupendana ni jambo la heri na la kupendeza sana.Hata maandiko yanatuasa tupendane. Lakini inabidi tuwe makini katika hilo maana huyo huyo umpendae anaweza kukugeuka siku yoyote. Hapo unaweza hata kujutia ulichokuwa umemfanyia huko nyuma. Uzoefu pia unaonyesha kuwa unaweza ukamchukia sana mtu lakini baadaye akaja kuwa wa msaada sana kwako siku ukipata shida.
Duniani Kuna Watu Waliondaliwa Maisha Na Wanaojiandalia Maisha
Msemo huu unazungumzia uhalisia wa maisha katika dunia hii tunayoishi. Wako watu wanaishi kutokana na hali ya wale waliowatangulia. Kama wazazi au walezi walikuwa na jina la kusifika, basi kizazi kinachofuata kitatembea katika hali ile ile. Kwa mantiki hii,?watakuwa wepesi kuonekana katika eneo lolote lile kutokana na majina makubwa wanayotembea nayo. Mfano kwenye siasa watoto wa wenye majina ni rahisi kufikiriwa na kupata kile wanachokitaka, pamoja na kazi nzuri, kisa tu, jina kubwa linawalinda.
Kushindwa Ni Sehemu Ya Maisha
Wengi wetu katika maisha, kuna mambo ambayo huwa tunapanga kuyafanya. Unaweza kupanga kwa muda wa dakika tano au kumi, inategemea, haijalishi. Kwa mfano, mtu akienda shule mpaka chuo, kwa kawaida anategemea kuwa akimaliza masomo yake atakuwa mtu mkubwa na mwenye nafasi katika jamii yake.
Akumulikaye Mchana Usiku Hukuchoma
Maadam tunaishi hapa duniani, tunakutana na marafiki wazuri, wabaya, wanafki, wambea na wengine wengi tu. Kwa mfano, rafiki yako unayemwamini sana anaweza kukutania, kukutishia au kukusema vibaya hadharani, yaani waziwazi, lakini kwa kuwa ni rafiki yako mmeshibana, unaona ni utani au kawaida tu, na unaweza ukamchukulia poa.