La Kuvunda Halina Ubani
Katika maisha ya ndoa kuna misukosuko mingi. Mingine inavumilika na mingine haivumiliki. Ninachotaka kusema hapa ni kwamba katika kupendana kwa nyie wawili mara nyingi si nyote wawili mnakuwa mnapendana kwa dhati, yaani kupendana kwa hali na mali.
Usipime Umuhimu Wa Mtu Kwa Mahitaji Yako
Binadamu kwa kawaida, tunaishi kwa kusaidiana. Inaweza ikatokea katika maisha yako ukawa na mtu ambaye kwako wewe ni msaada mkubwa. Pengine ni yeye anayekusaidia katika shida zako mbalimbali. Mtu huyo unaweza ukamuona kuwa ni rafiki au ndugu kwa sababu huwa ni kawaida yake kukusaidia siku zote. Kwa kifupi, mtu huyu tunaweza kusema kuwa ni mkombozi wako kwa kila hali.
Matumizi Ya Teknolojia Ya Simu Yaleta Msaada Kwa Mama Na Mtoto
Katika kufanya kazi zake, "TEWWY" (Tap Elderly Women's Wisdom for Youth), haiko mbali na kauli mbiu ya Kimataifa na Kitaifa ya Siku ya Wanawake Duniani 2023. Kauli mbiu hiyo ya "Ubunifu na Mabadiliko ya Teknolojia, Chachu kuleta Usawa wa Kijinsia
Maji Ya Moto Hayaunguzi Nyumba
Maji ya moto katika usemi huu, tunamaanisha maneno maneno hayavunji mfupa. Ni kawaida kabisa kila siku iendayo kwa Mungu sisi binadamu, muda mwingi tunautumia kwa kusemana semana na kufanyiana vurugu nyingi za hapa na pale. Hata pale inapoonekana kuwa mtu anajihangaisha bila kuchoka ili kujitafutia riziki yake, vimaneno maneno huwa ni vingi sana
Tuwe Tayari Kufanya Kazi Wakati Wote
Kinachofuata ni kisa cha mama na mtoto wake wa kiume. Yaliyomo ndani ya kisa hiki yanaweza yakakuumiza sana kama una roho yenye huruma na ya kibinadamu
Nyoka Na Jongoo
Hapo zamani za kale, Nyoka alikuwa ana miguu lakini macho hakuwa nayo. Jongoo naye alikuwa na macho, lakini miguu alikuwa hana
Ukomo Wa Subira Yako Ndio Mwanzo Wa Husuda
Kila jambo linalofanywa na mtu yeyote lina mahali pa kuanzia. Katika kuanza jambo kunahitajika mipango thabiti ili liweze kutekelezeka. Utekelezaji wa mipango hiyo, utahusisha binadamu wengine kwa asilimia kubwa. Kwa kawaida, kipindi hicho huwa ni cha mpito
Wazazi Wana Haki Ya Kutunzwa Na Watoto Wao
Kinachofuata ni kisa cha mama na mtoto wake wa kiume. Yaliyomo ndani ya kisa hiki yanaweza yakakuumiza sana kama una roho yenye huruma na ya kibinadamu
Acha Kuishi Kwa Wasiwasi, Hapo Ulipo Bado Una Nafasi
Maisha ni kupanda na kushuka. Chochote utakachokifanya, ni lazima utapitia changamoto za aina mbali mbali. Changamoto hizo zisikufanye uishi kwa wasiwasi na pia zisikukatishe tamaa.
Tutumie Mikakati Thabithi Katika Kuwafunza Watoto Wetu Maadili Mema
Hapo zamani kulikuwa na kaka mmoja ambaye alikuwa akiwalea dada zake wawili. Aliwapenda sana na akawa karibu nao. Aliwalea vizuri na kuwapatia mahitaji yao ya msingi
Mtoto Umleavyo Ndivyo Akuavyo
Mithali hii ni ya msingi sana, kuanzia pale mtoto anapozaliwa kwani tabia ya mtu inaweza kuwa nzuri au mbaya kutegemea na alivyolelewa na kukuzwa. Mfano, kama baba anakuwa na tabia ya kufokafoka na ukali uliopitiliza kila anaporudi nyumbani, watoto wake huishi kwa kuogopa muda wao wote. Pia wanaweza wakajenga tabia ya kuwa na hofu kila wakati wanapomuona baba yao. Woga ukiwazidi pia huwafanya watoto kuwa na tabia ya uongo na hata ya unafiki. Watoto wana akili sana. Wanaweza wakaamua kuwa vile mzazi wanavyomuona anataka wawe
Mtandao Ni Uwanja Wa Ulaghai
Baadhi ya wasichana wamekuwa wakirubuniwa na baadhi ya wanaume wanaoishi nchi za nje. Warubuni na warubuniwa, hukutana kwenye mitandao ya kijamii. Utandawazi ndio chanzo kikubwa cha kuleta yote haya. Mahusiano huanzia hapo, kwenye mitandao, juu kwa juu
Fanya Kazi Vizuri Kwenye Nafasi Yako
Kazi ndio msingi wa maisha. Binadamu sote hujishughulisha na kazi ili waweze kuishi. Katika mchakato huo wa kufanya kazi, unakutana na watu wengi ambao nyote mpo kwa ajili ya kufanya kazi na kupata riziki
Mchumia Juani Hulia Kivulini
Mchumia juani ni mtu anayetafuta riziki kwa kufanya kazi, biashara au ujasiriamali. Jitihada hizo hufanywa kwa bidii. Kulia kivulini ni mafanikio au matunda anayopata baada ya kazi ngumu
Kilio Cha Mbuzi Hakimzuii Kupelekwa Sokoni
Hapa duniani, kuna matukio mengi sana ambayo yanatukuta kila siku za maisha yetu sisi wanadamu. Matukio mengine huumiza na mengine yanafurahisha. Dunia ndivyo ilivyo. Endapo matukio yote yangekuwa yanafanana, kwa hakika yangeweza kutuchosha, wengine husema, yange-boa
Kawia Ufike
Kukawia ni kuchelewa au kutofika kwa wakati unaotakiwa. Wanaposema kawia ufike wana maana chelewa lakini ufike mahali unapotakiwa kuwa. Msemo huu unatumiwa sana na baadhi ya watu wasiojitambua na wasiokuwa na uhakika wanatakiwa wafanye nini. Sehemu za ibada ni moja za sehemu ambazo watu hutumia sana msemo huu. Wanapoutumia msemo huu kwenye masuala ya nyumba za ibada, wanakuwa na maana kuwa hata wakikawia, ili mradi watakuwa wamefika, haijalishi sana. Kwa wanaosema hivi ina maana kuwa, cha muhimu kwao ni kuonekana kuwa walikuwepo ili mradi wasieleweke vibaya
Mwamini Mungu Si Mtovu
Alikuweko mtu mmoja na mkewe, hawakuwa na kitu, rasilimali yao kubwa ilikuwa ni kondoo na jogoo. Siku moja walipata habari kuwa rafiki yao alikuwa anakuja kuwatembelea. Mke alimwambia mume wake kuhusu ugeni huo. Alimkumhusha kwa kusema kuwa walikuwa hawana kitu chochote cha kumkirimu mgeni wao. Walichokuwa nacho ni huyo kondoo na jogoo. Lakini, mke aliongeza kuwa yeye asingependa kuwachinja wanyama wake, yaani kondoo jogoo
Kaa Mbali Na Mazoea
Maisha yetu katika ulimwengu huu ni ya vurugu kati ya mtu na mtu. Chochote mtu akifanyacho kimeanzia kwenye fikra zake. Kwa kawaida, mtu hawezi kukurupuka tu na kuanzisha kitu bila kufikiria na kupembua kama hilo jambo litawezekana ama la. Mara nyingi, tunafanya kosa kumshirikisha mtu ama watu mawazo yetu mapema mno. Inawezekana, huyo unayemshirikisha hawezi kukutia moyo ili ufanikiwe, binadamu wengi ndivyo walivyo. Wengi hupenda kukatisha tamaa wenzao na hata kunena maneno mengi ambayo yanaweza kukutoa kwenye wazo lako.
Fikra Zako Usimshirikishe Mtu
Maisha yetu katika ulimwengu huu ni ya vurugu kati ya mtu na mtu. Chochote mtu akifanyacho kimeanzia kwenye fikra zake. Kwa kawaida, mtu hawezi kukurupuka tu na kuanzisha kitu bila kufikiria na kupembua kama hilo jambo litawezekana ama la. Mara nyingi, tunafanya kosa kumshirikisha mtu ama watu mawazo yetu mapema mno. Inawezekana, huyo unayemshirikisha hawezi kukutia moyo ili ufanikiwe, binadamu wengi ndivyo walivyo. Wengi hupenda kukatisha tamaa wenzao na hata kunena maneno mengi ambayo yanaweza kukutoa kwenye wazo lako.
Elimu Bila Vitendo Ni Sawa Na Bure
Elimu ni maarifa anayopata mtu darasani. Vijana wengi wamepata elimu wakianzia chekechea hadi vyuo . Baadhi yao elimu hiyo imewasaidia, wakafanikiwa na wengine kwa bahati mbaya walishindwa