Binadamu Ana Nyuso Mbili, Kaa Nae Kwa Akili
Mara nyingi tumeona kuwa siyo watu wote wanaokuzunguka ni wema kwako. Wewe unaweza ukajiona kuwa ni mwema kwa watu na wao , vivyo hivyo, ukawaona ni wema kwako. Katika imani hiyo unaweza ukajiridhisha na kuona kuwa una ndugu au marafiki wa haja, marafiki wa kukimbiliwa ukiwa na shida.
Kisa Cha Kuku Na Kanga
Hapo zamani kuku walikuwa ndege wa mwituni. Waliishi pamoja na kanga na ndege wengine. Basi siku moja ikaja mvua kubwa huko mwituni. Kanga akamwambia kuku, nenda kwa binadamu ukaombe moto ili tuje tuote. Baridi imezidi, ni kali sana. Kuku alitii agizo la kanga. Alienda, na alipofika kwa binadamu, alikaribishwa vizuri. Binadamu alimuuliza shida iliyompeleka hapo.