
Tuwe Wastaarabu Na Busara Katika Maongezi
Binadamu tunatakiwa kuishi kwa kufuata taratibu fulani zilizopo kwenye jamii, hii ni pamoja na jinsi tunavyozungumza na wenzetu. Kwa maana hiyo, ukiwa mstaarabu na mwenye busara huwezi kuuliza uliza watu maswali ambayo hayastahili kuulizwa, maswali kama: ‘Bado hujaolewa tu?….Una watoto wangapi?…Utazaa lini?…Mbona umri umeenda?…na mengine mengi.
Hekima Ni Jambo La Msingi
Kile unachokiita baraka au ushindi kilianza kama tatizo. Mara nyingi, yule anayefanikiwa kutatua matatizo huonekana kama ana baraka au mshindi fulani hivi. Ni kawaida kwa kila mwanadamu kupata matatizo. Pale mtu anapopata matatizo, ni vema kutafuta mbinu za kupambana nayo. Wengi hujaribu kukimbia matatizo yanapotokea.

Mafanikio Makubwa Yana Vikwazo
Njia nyepesi kabisa ya kutofika popote ni kusubiri ueleweke na kusifiwa na kila mtu kwa jambo uliloamua kulifanya. Uhalisia ni kwamba huwezi kueleweka kwa kila mtu na sio rahisi sana kusifiwa na kila mtu hasa jambo linapokuwa katika wazo ama hatua za awali.

Mchumia Juani Hulia Kivulini
Mchumia juani ni mtu anayetafuta riziki kwa kufanya kazi, biashara au ujasiriamali. Jitihada hizo hufanywa kwa bidii. Kulia kivulini ni mafanikio au matunda anayopata baada ya kazi ngumu















