Maisha Mashenzi
Maisha ni zawadi ambayo Mungu ametupa wanadamu ili tuishi kwa mafanikio kadiri alivyotuahidi maana vyote chini ya jua ni vyetu kwa hiyo kila mtu awe na maisha mazuri na yenye baraka.
Penye Mafanikio Kuna Furaha
Shughuli yoyote ambayo mwanadamu anafanya ni kwa madhumuni ya kufanikiwa. Katika mafanikio hayo ndipo inazaliwa furaha. Daima ukiona mtu amefurahi sana, ukitafuta sababu utakuta kuwa kuna mahali amefanikiwa. Nyumba yeyote ambayo imejaa upendo, basi elewa kuwa pale pana mafanikio kwa njia moja au nyingine.
Heri Lawama Kuliko Fedheha
Lawama ni hali ya kulalamika kuhusu jambo ama tatizo fulani. Fedheha maana yake ni aibu. Mara nyingi watu hutumia muda wao mwingi kulalamikia ugumu wa maisha. Ukiwachunguza watu hao kwa undani utakuta ni wale ambao ni wavivu, wasiopenda kufanya kazi. Mara nyingi watu hao hushinda vijiweni na kuzungumza mambo ya umbea ambayo hayana tija kwao wala kwa jamii. Kati ya watu hawa huwa na dharau na kebehi, wasiotafuta fursa, wasiopenda kushirikiana na wenzao na wenye mtizamo hasi dhidi ya wenzao na wao wenyewe.
Mawazo Ya Watu Wenye Hekima Ni Kama Shamba
Hekima ni mojawapo ya vipaji ambavyo Muumba wetu hutoa kwa viumbe wake. Ieleweke kuwa, sio kila mtu anajaliwa kupata vipaji. Lakini endapo itatokea kuwa unataka kipaji basi unashauriwa kuwa ni vema ukaomba hekima.
Ziba Mwanya Usiruhusu Panya Kupita
Mwanya ni nafasi yoyote ambayo mtu au kitu kinaweza kupita au kupenyeza bila kizuizi. Unaweza kuwa mwanya mkubwa au mwanya mdogo, alimradi hauzuii kilichokusudiwa kupenyeza. Hii ina maana kuwa, jambo lolote linapoanza kuharibika, huanza kidogo kidogo au taratibu sana na wakati mwingine bila hata kutambua.
Mwongo Huwa Hasemi Yake
Mtu mwongo ni yule mtu ambaye anapenda kuongea mambo ya wenzake kwa ushabiki. Mara nyingi huwa anaongea katika mithili ya kumdhalilisha mtu. Watu wa aina hii huwa wana asili ya kuwa na marafiki wengi ambao huvutiwa na stori zake za uongo. Huo ni ubinadamu wa watu ambao hawajitambui. Mara nyingi, kinachofanyika hapo huwa ni unafiki mtupu.
Muda Haumsubiri Mvivu
Kila jambo lina wakati na majira yake. Hata tunapopanga mipango tunaweka na muda wa kutekeleza. Pamoja na hayo, inategemea na jinsi wewe mpangaji wa mipango kama unajali muda na wakati wa kuitekeleza. Usipozingatia utakuta muda umeondoka bila ya matokeo.
Akufaaye Kwa Dhiki Ndiye Rafiki
Kulikuwa na bawana mmoja ambaye alitaka kujua rafiki yake wa kweli ni nani. Siku moja alimwambia mkewe, "Mke wangu andaa chakula kizuri na kingi. Nataka kula na rafiki zangu wapenzi". Mkewe alifanya kama alivyoamriwa na mumewe. Akanunua kila aina ya mapochopocho na kupika. Pia alinunua vinywaji vingi vya kutosha kwa ajili ya wageni wake.
Tafuta Raha, Shida Zinakuja Zenyewe
Neno shida lina maana pana sana. Tunaweza kusema kuwa shida ni tatizo ambalo mtu anakuwa nalo. Mtu anaweza asijue namna ya kujinasua au namna ya kufanya ili aondokane nayo.
Usiogope Kuchukiwa, Ogopa Kulaumiwa
Chuki na lawama ni mambo ambayo yanakuja kwa kasi sana katika maisha ya jamii zetu. Mbaya zaidi, katika mahali pa kazi, hayo yameanza kuwa ndio maisha ya wengi. Kwenye sehemu ya kazi, chuki huja kuhusiana na utendaji wa kazi wa mtu. Kuna ambaye anachukiwa tu kwa sababu ya utendaji wake wa kazi na umakini katika kuitenda kazi aliyokabidhiwa na mkuu wake wa kazi.
Hakuna Marefu Yasiyokuwa Na Ncha
Maisha ni mzunguko, na sisi binadamu tunapoishi hapa duniani, tunakutana na mambo mengi sana yakiwemo mazuri na mengine mabaya, ya kusikitisha na hata yanayofurahisha.
Ukubwa Ni Jaa
Jaa ni jalala, mahali ambapo watu hutupa taka taka zao. Kwa hiyo mtu mkubwa ni kama jaa, kila mwenye takataka zake, (matusi, lawama, n.k) humtupia yeye.
Adui Hatoki Mbali
Usemi huu unatufundisha jinsi tunavyopaswa kuishi na jamii na marafiki wanaotuzunguka. Ni vizuri kuwa karibu na hao watu kwa sababu hata maandiko yamesema binadamu tupendane na tusaidiane. Tunapaswa kujua kuwa hayo yote tunatakiwa tuyafanye kwa kiasi na kwa makini sana. Kumbuka, wema wako unaweza kukupeleka kwenye kilio. Sio kilio cha kufiwa, bali tunaongelea kilio kitokanacho na matatizo utakayoyapata baada ya hapo.
Usitunze Huzuni Moyoni
Huzuni ni hali ya masikitiko yenye masononeko inayomfanya mtu akose furaha, amani na matumaini kwa kiwango kikubwa na kwa muda mrefu. Hali hiyo humfanya mtu atawaliwe na mawazo mengi sana, ikiwa pamoja na msongo wa mawazo na sonona. Inapokithiri bila kupata huduma sahihi huweza kusababishahta kifo.
Usitoe Maamuzi Wakati Una Furaha Sana
Tuko katika ulimwengu wenye vurugu na fujo zisizohesabika. Kila mtu anacho akijuacho ambacho anaona mwingine hakijui na wala hakiwezi. Ni fikira ambazo wanadamu tunatembea nazo. Furaha na huzuni ni sehemu ya maisha yetu.
Mtu Hufurahia Shida Zako, Sio Furaha Yako
Matatizo yameumbwa na kila mtu huyapata. Hakuna mtu ambaye hajawahi kupitia matatizo, na hayuko ambaye hatayapitia. Inategemea ni tatizo gani na wakati gani linakutokea.
Ishi Kadri Unavyojaliwa, Na Sio Kama Mwingine Anavyoishi
Watu wengi wana kawaida ya kupenda kujilinganisha na watu wengine. Watu kama hao hupenda kujiuliza, “kama yule yuko hivi, kwa nini na mimi nisiwe vile?”
Tujifunze Kusamehe
Alikuwepo mama mmoja ambaye alikuwa mwalimu wa shule ya msingi. Mama huyu alibahatika kupata mtoto wa Kike ambaye aliweza kumsomesha hadi Chuo Kikuu. Baada ya kuhitimu shahada yake, alimtafutia kazi nzuri.
Njia Ya Mkato Tamu, Lakini Ina Madhara
Mara nyingi kama mtu anataka afike haraka, anatafuta njia ya kukatisha, njia ya haraka. Njia hiyo inaweza kuwa nzuri pale tu utakapofanikiwa kufika kule uendako. Kuna wakati lakini njia ya mkato inaweza ikakupoteza na ukashindwa kufika uendako. Kuna baadhi ya binadamu, hupenda kutafuta mafanikio kwa kupitia njia ya udanganyifu, kama kutapeli wenzao.
Tuwe Wastaarabu Na Busara Katika Maongezi
Binadamu tunatakiwa kuishi kwa kufuata taratibu fulani zilizopo kwenye jamii, hii ni pamoja na jinsi tunavyozungumza na wenzetu. Kwa maana hiyo, ukiwa mstaarabu na mwenye busara huwezi kuuliza uliza watu maswali ambayo hayastahili kuulizwa, maswali kama: ‘Bado hujaolewa tu?….Una watoto wangapi?…Utazaa lini?…Mbona umri umeenda?…na mengine mengi.