
Jifunze Kutotangaza Shida Zako
Tatizo au shida humpata mwanadamu yeyote hapa duniani. Huo ndio ukweli wa maisha, kwani maisha ndivyo yalivyo. Kawaida, mtu akipata tatizo, hali yake hubadilika na tunaweza tukasema kuwa, mtu huyo huwa hayuko sawa. Anaweza akatafuta namna ya kutoka au kulitatua jambo linalomsibu. Kufanya hivyo ni hali ya kawaida sana.

Anayetembea Kwenye Matope Yampasa Asafishe Miguu Yake
Hapa duniani kuna aina nyingi za barabara. Kuna barabara zile za lami, moramu na vumbi. Ikitokea umetembea kwenye barabara ya vumbi na mvua ikawa imenyesha, utakanyaga matope.

Kuku Mgeni Hakosi Kamba Mguuni
Kuku ni ndege afugwaye kwenye makazi ya wanadamu. Kuku huchukuliwa kuwa ni kitoweo cha heshima kwa wageni wa hapo majumbani kwa watu.

Mkuki Kwa Nguruwe, Kwa Binadamu Mchungu
Mkuki ni silaha ya jadi inayotumika kuwinda wanyama wakubwa. Hapa kwenye msemo huu ina maana kuwa maneno makali ya kuumiza, kudhuru na kubomoa, kwetu sisi wanadamu inaonekana kuwa, ukimtamkia mtu mwingine unaweza kuona ni kawaida na sawa. Lakini maneno hayo hayo ukitamkiwa wewe utaona kuwa ni mabaya na utachukia kupindukia.

Kikulacho Ki Nguoni Mwako
Neno kikulacho linaelezea uharibifu ambao unaweza kutokea au kufanyika kwa makusudi au bila kukusudia ili kumuharibia mtu. Mara nyingi hilo jambo hutokea kwa watu wanaoelewana vizuri. Zaidi ni marafiki ambao huwa wanafanyiana hivyo. Hii ni kwa sababu kila mmoja anamuelewa mwenzake vizuri. Inawezekana akawa ni jirani yako au ndugu yako.

Unachokifanya Leo Kinatengeneza Kesho Yako
Jambo lolote ambalo mwanadamu analifanya linategemea sana maandalizi aliyojiwekea kwenye mipango na mikakati yake. Mafanikio hayawezi kuja kwa kufikiria tu, bali ni kwa utekelezaji wa yale uliyojipangia.

Wagombanapo Ndugu, Chukua Jembe Kalime, Wakipatana, Chukua Kapu Kavune
Ndugu ni watu waliozaliwa katika familia moja au ukoo mmoja. Ugomvi ni hali ambayo hujitokeza kwa kutokuelewana mtu na mtu. Ugomvi huu unaweza ukafikia hata kupigana.

Shida Haipigi Hodi
Shida ni tatizo au changamoto inayomfika mwanadamu. Hodi ni neno linalotumika badala ya swali la: “naweza kuingia?" Hapa anaposema shida haina hodi sio kweli maana mwanadamu anapopatwa na tatizo ataingia kwa jirani na kutoa shida zake ikibidi kuomba msaada ili atatue changamoto zake. Shida inaweza kukupeleka hata mahali ambapo hujawahi kufika.

Upendeleo Au Ubaguzi Ndani Ya Familia Siyo Mzuri
Watoto ni zawadi kutoka kwa Mungu, hivyo tunapaswa kushukuru. Mungu anapokupa watoto wawe wa kiume, kike au mchanganyiko inabidi uridhike na kumshukuru Mungu, kwani kuna wengine ambao hawakujaliwa kupata kabisa.

Utaula Wa Chuya Kwa Uvivu Wa Kuchagua
Chuya ni mpunga ambao unakuwa umejichanganya na mchele mzuri ambao upo tayari kwa kupikwa. Hizo chuya huwa zinatakiwa kuchaguliwa ili kupata mchele mzuri, tayari kwa kupikwa. Lakini inawezekana kwa watu wengine ambao ni wavivu, kuupika mchele ukiwa hivyo haujachaguliwa wasione tofauti ama vibaya.

Furaha Ni Kama Marashi Kwani Huongeza Maisha
Wahenga wa kale walisema, "Kitu furaha ni sawasawa na marashi”, kwani huwezi kujipulizia wengine wasisikie harufu yake. Hii inajidhihirisha wazi kwamba ukiwa na furaha huwezi kuificha kwani mtu yeyote atakayekuona atatambua kuwa umefurahi au una furaha. Basi, endapo wewe umefurahi, jitahidi na watu wengine nao wafurahi kutokana na furaha yako.

Usitegemee Uzuri Wako Maana Kuna Siku Utazeeka
Wako mabinti zetu wengi ambao wanajiona ni wazuri kwa umbo na sura. Watu hao mara nyingi hujiona kuwa ni bora zaidi kuliko wengine. Na huwa wanapenda hata kuchagua ni nani watakuwa wenzi wao.

Anayekukosoa, Anakujenga!
Ni kawaida ya watu wengi kupenda kuonekana kuwa wako mbele sana katika kila jambo wanalolifanya. Hakuna mtu anayetaka kuonekana kuwa hawezi.

Maisha Ni Kutegemeana
Maisha ya mtu ni fumbo zito. Kila mtu ana umuhimu katika maisha ya mwenzake. Hii ni kwa sababu maisha ni kutegemeana.

Wakati Mwingine Hawakupendi, Wanakupenda Kwa Kile Ulicho Nacho
Ni ukweli usiopingika kuwa watu humpenda mtu mwenye nacho. Watu wa aina hii, yaani wale wenye nacho, huwa na marafiki wengi kupita maelezo. Ukweli huu huonekana zaidi kama huyo mtu atakuwa ni mtoaji sana na ambaye anapenda kusaidia watu.

Heri Shetani Unayemjua, Kuliko Malaika Usiyemjua
Tupo duniani tukizungukwa na watu mbalimbali na wenye tabia tofauti tofauti. Tunaishi kwa kutegemeana maana sisi ni wanadamu ndiyo maana utaona watu wanasaidina kwa shida na raha. Zaidi ya hapo utaona kwenye jamii zetu, kuna watu wanaishi kwa kupendana kama ndugu na kufanya vitu pamoja na kushauriana kwa kila jambo linalokuja mbele zao.

Usitumie Usomi Wako Kuwanyanyasa Na Kuwatambia Wenzako
Wako watu wanaojiona, wanaojitapa na kutamba kuwa wana akili sana. Hujiona wamesoma na wameelimika zaidi ya wengine. Watu hawa huchukua fursa hiyo ya kuelimika kama fimbo ya kuwachapia wenzao. Huwanyanyasa wenzao kwani huwaona kuwa ni wajinga na pia hawana elimu. Hali kadhalika, huwadharau, kiasi kwamba hata kuongea nao inakuwa ni shida, kisa, eti hawajasoma.

Mpatie Mtu Ujira Wake Kwa Wakati Anaostahili
Kuna aina nyingi za ajira hapa duniani. Usemi huu unawalenga wale tunaowaajiri hasa kwenye kazi za nyumbani (house girls). Kuna tabia mbaya ya baadhi ya waajiri kwenye sekta hii kutokuwajali na kuwathamini wafanya kazi wa sekta hii.

Yatima Hadeki
Neno yatima au ukiambiwa yule ni yatima kila mtu ataelewa. Yatima ni mtoto ambaye, aidha kafiwa na mzazi mmoja au kafiwa na wazazi wake wote wawili.

Usimtekenye Aliyekubeba, Atakudondosha
Maisha yetu ni ya kutegemeana kwa kiwango kikubwa sana. Hakuna mtu atakayesema hapa alipo amefika kwa juhudi zake mwenyewe. Lazima kuna mahali alifika akakwama, na mtu mwingine akamkwamua na hatimaye akatoka.