
Kumbuka Kuna Kesho
Unapoishi na watu hapa duniani, tambua kuwa kuna kesho. Aidha, unapokuwa kiongozi wa watu sehemu fulani kumbuka pia kuna kesho. Unapokuwa na madaraka, nafasi ya juu, kipato kizuri, na mwenye kutoa maamuzi ya juu, kumbuka kuna kesho.
Kua Makini, Chunguza Ushauri Unaopewa Kabla Ya Maamuzi
Ushauri ni maoni yanayotolewa kwa mtu ili yamsaidie kupata suluhisho kwenye changamoto anazopitia. Aidha, ushauri ni maelekezo ya kitaalamu yanayotolewa kwa mtu yeyote ili kumwezesha kufanya jambo fulani.

Hakuna Mtu Duniani Anayeweza Kuziba Pengo La Mtu Mwingine
Duniani kila mtu alikuja kwa wakati na majira yake. Hata mapacha waliigia duniani kwa muda tofauti. Kila mtu amekuja duniani kwa kusudi lililopangwa na Muumba wake. Katika hali hiyo hiyo basi, kila mtu ataondoka kwa wakati wake. Haijalishi kama mlizaliwa mapacha. Hii ina maana kuwa mmoja akiondoka, linabaki pengo lisilozibika.

Jifunze Kujishusha Machoni Pa Watu Wengine
Baadhi ya watu wana ile tabia ya kuona kwamba wao ndio pekee wa kuweza kutoa maamuzi ya aina yoyote wakiwa kwenye kundi la watu. Tabia ya watu hawa ni ya kujiona na kujisikia kuwa wao ni bora kuliko watu wengine. Watu hawa hufikia hatua ya kuchukia pale wanapotoa jambo/ushauri mbele za watu na halafu usikubaliwe. Huwa hawaelewi kabisa kwa nini yale wanayosema yasikubaliwe na watu.

Ujana ni Dhahabu
Katika maisha tunaweza kusema kuwa, "umri wa ujana" ni kipindi cha dhahabu ambacho tunatengeneza marafiki wengi na kupoteza wengi pia. Katika kipindi hiki, uamuzi wa kuyaharibu au kuyatengeneza maisha yako ili yawe mazuri baadaye unao wewe mwenyewe. Kwa hiyo inakupasa kukumbuka kuwa kipindi hiki kikishapita hakijirudii tena. Hivyo kitumie vizuri uwezavyo.
Usitoe Maamuzi Wakati Una Hasira
Hasira ni ile hali ya kuhamaki kwa jambo ambalo umesikia au umefanyiwa na mtu bila kukubaliana ama kuridhika nalo. Inawezekana likawa ni jambo la kusingiziwa au la. Hasira inaweza kukupelekea kuamua chochote kibaya, ukafikia hata hatua ya kuua. Mara nyingi hasira inaishia kwenye kujuta kwa lile ulilolifanya kwa kukusudia ama kutokusudia. Sambamba na usemi huu ni ule wa Majuto ni Mjukuu. Tunaaswa kutokuamua jambo lolote wakati tuna hasira.

Heri Nitakula na Nani Kuliko Nitakula Nini
Maisha tuishio yapo katika matabaka tofauti. Wapo watu wenye uwezo sana, wapo wale wenye uwezo wa kati na wale wenye uwezo wa chini. Ni muhimu kujua kuwa maisha yetu sisi binadamu yanatofautiana.

Ukipanda Cheo Usisahau Familia Yako
Cheo ni aina mojawapo ya usitawi au baraka azipatazo mwanadamu katika mazingira yake ya kazi. Hata mfanya biashara anapokuwa amekua kibiashara, nako pia ni kama kupanda cheo.

Kinga ni Bora Kuliko Tiba
Kinga ni kudhibiti tukio au jambo kabla halijaleta madhara. Tukio linaweza kuwa ni ugonjwa au mambo mengine yawayo.

Tunza Siri za Kazi Zako kwa Mafanikio Yako
Hapa duniani kuna baadhi ya watu wenye makelele na fujo nyingi ambao hujigamba bila hata kuulizwa maswali yanayohusu kazi wazifanyazo.

Maisha ni Mafupi, Tusiache Kutenda Mema
Kutenda mema au wema ni silaha kubwa katika maisha yetu. Kuishi hapa duniani ni kwa neema tu ambayo mtu hujaliwa na Muumba wetu. Hatuna uhakika na siku zetu za hapa duniani. Hatuna uhakika kama tutamaliza salama siku zetu zilizosalia ama laa, hiyo ni siri ya Mwenyezi Mungu pekee.

Mvuvi Ajua Pweza Alipo
Mvuvi ni mtu anayevua samaki kwa ajili ya biashara. Akifanikiwa kupata samaki wengi, wengine huwaacha kwa ajili ya matumizi ya nyumbani. Hiyo ndio kawaida ya wavuvi. Pweza ni samaki anayependwa sana na watu hasa watu waisio ukanda wa pwani. Pweza huwa wanauzwa kwa bei mbaya sana.

Nyakati Ngumu Ndio Thibitisho la Ujasiri Wako
Nyakati ngumu ni kipindi ambacho kila mtu hupitia katika maisha yake. Katika kipindi hicho, inawezekana hali ya uchumi ikawa imeyumba na kuyafanya mambo yasiende ipasavyo. Kama una ujasiri, hali hiyo haitakuchanganya bali utaendelea kuwa na amani. Lakini usipokuwa jasiri, kila mtu ataelewa kuwa unapitia kwenye hali ngumu, hiyo haitakuwa sahihi hata kidogo.

Mpende Adui Yako
Adui ni mtu ambaye huna mahusiano mazuri naye. Mtu huyu utamtambua kuwa ni adui kwa matendo yake na hata kuongea kwake. Mara nyingi adui yako kila atakaloongea kwako huwa ni hasi na pia huwa halina amani.

Udhaifu Wako Usikufanye Ujiwekee Ukuta Kuzuia Mafanikio
Wakati mwingine binadamu tunakuwa na tabia ya kujidharau na kutojipenda. Huwa tunafikia hata hatua ya kujikataa na kujiona hatufai. Hali kadhalika, hujiona kuwa hatustahili kuishi na kwamba hata tukifanya kazi yoyote hatuwezi kupata mafanikio. Kuna wakati huwa tunakuwa na mtizamo hasi dhidi ya maisha yetu sisi wenyewe.

Maneno si Mkuki
Ulimi hutamka maneno yaani silabi zilizounganishwa zikaleta tamshi la kueleweka. Mkuki ni silaha ya jadi ambayo imetengenezwa kwa mti na ncha kali ya chuma. Mkuki hutumika kuwindia wanyama, hususani, wanyama wakubwa.

Heshima Hutengenezwa kwa Hekima, Haitengenezwi kwa Mkiki
Mara nyingi tunapenda kumsifia mtu tunapoona kuwa ana heshima. Lakini hatuelewi kwa nini huyo mtu yuko vile alivyo. Silaha kubwa juu ya hilo ni hekima.

Mgeni Njoo, Mwenyeji Apone
Mgeni ni mtu anayekuja kwenye makazi ambayo hana mazoea nayo au ni mahali ambapo siyo kwake. Kwa kawaida, mtu huyu anapokuja humfanya mwenyeji wake kuhangaika kutafuta hiki na kile, ili mradi yeye na mgeni wake waweze kufurahi pamoja. Mgeni huyo anaweza kuwa ni ndugu ambaye ametoka mbali kuja kusalimia tu ama kwa shughuli nyingine.

Ni Rahisi Kubeba Kikombe Kisicho na Kitu Kuliko Kile Chenye Kitu
Kwenye maisha ya binadamu, tunaposema “Ni rahisi kubeba kikombe kisicho na kitu kuliko kikombe chenye kitu“, ina maana kubwa. Kwa mfano, ukiishi na watu mbalimbali huku ukijivuna, ukiwadharau na kuwaona hawafai, hawajui kitu, ila wewe unajihesabia kuwa ndiye unayejua kila kitu, watu watakulinganisha au watakufananisha na kikombe kisicho na kitu chochote ndani yake, yaani kikombe kitupu.

Kuvunjika kwa Koleo, Sio Mwisho wa Uhunzi
Uhunzi ni shughuli za ufundi chuma. Koleo ni chombo kinachotumika na mafundi wanaojishughulisha na masuala ya chuma. Endapo katika kukata chuma kikavunjika, kitakachofanyika ni kwenda kutafuta chuma kingine ili kazi iendelee.