
Kama Hukushiba Kwenye Tonge, Kwenye Kulamba Utajisumbua Tu
Mbiu ya maisha huanzia mapema. Kama mwanzo wa safari yako haukuwa mzuri, unaweza ukafika uendako kwa matatizo au kwa shida sana.

Bandu Bandu Humaliza Gogo
Maisha ni safari ndefu sana ambayo imejaa mapito mengi mazuri na mabaya. Unaweza ukapitia eneo ambalo ni la kukukatisha tamaa hata ukakosa jawabu.

Mwenye Shoka Hakosi Kuni
Kuna watu ambao wamejijengea tabia ya kupokea tu kutoka kwa wenzao, lakini wao sio wepesi wa kutoa kabisa. Watu wa namna hii, kupokea kwao huwa ni rahisi, lakini inapofika kwa wao kutoa, wanakuwa hawako tayari kabisa kufanya hivyo. Ukweli ni kwamba hata huwa hawakumbuki kurudisha fadhila walizotendewa na wengine.

Wanao Subiri Anguko Lako Ni Wengi Kuliko Wanaosubiri Mafanikio Yako
Kwenye dunia hii, kila mtu ana njia zake anazozifuata ili afanikishe maisha yake. Hali hii humpata kila mtu, awe baba au mama, lengo ni kuweza kumudu maisha ya hapa duniani. Kutokana na hali hiyo, wengine hufanikiwa kiurahisi na wengine huwa na mapito mengi kabla ya kupata mafanikio.

Kifo Ni Mali Ya Mungu
Maisha yetu yana mwisho, hii ni kwa kila mwanadamu. Kutokana na ukweli huo basi, hatuna ujanja wowote wa kukwepa kifo.
Epuka Marafiki Wanafiki
Kuna aina tofauti za marafiki. Kuna wale wanaojiona kuwa sahihi kwa kila kitu na bora zaidi ya wengine. Watu kama hawa hupenda sana kujisifu na kusifiwa pia. Watu wa aina hii, hata wakikosea hawakubali, bali hutengeneza mazingira ya kukufanya wewe uonekane kuwa ndiye uliyekosea.

Lawama Ni Kama Moshi
Katika mikusanyiko mingi ya watu, kuna mambo mengi ambayo hutokea. Kuna misuguano ambayo nayo hutokea kati ya mtu na mtu au kikundi na kikundi. Kulaumiana huwa ni kwingi sana kwa sababu kila mtu hujiona ana haki ya kusema chochote alichokuwa nacho, kiwe cha kweli au cha uongo.

Mzoea Kutwaa, Kutoa Ni Vita
Kuna watu ambao wamejijengea tabia ya kupokea tu kutoka kwa wenzao, lakini wao sio wepesi wa kutoa kabisa. Watu wa namna hii, kupokea kwao huwa ni rahisi, lakini inapofika kwa wao kutoa, wanakuwa hawako tayari kabisa kufanya hivyo. Ukweli ni kwamba hata huwa hawakumbuki kurudisha fadhila walizotendewa na wengine.

Akufanyiaye Ubaya.., Mlipe Wema
Mtu anayekufanyia ubaya ni yule anayekutendea jambo ambalo halikupendezi na ambalo linaweza kukuumiza kwa njia moja au nyingine. Mtu wa namna hii, hutakiwi kumlipa mabaya na wala usiwe na kisasi naye. Ikibidi, mtendee mema na usioneshe kuchukia wala kughadhabika.

Mwamba Ngoma, Ngozi Huvutia Kwake
Umaskini ni ile hali ya kuwa na uhitaji hasa wa yale mahitaji ya muhimu kama vile chakula na mengineyo mengi. Mtu wa aina hiyo huwa hawezi kukataa pale anapoomba, hata kama atakuwa amesemewa mbovu, yeye ataangalia uhitaji wake tu.

Subira Yavuta Kheri
Jambo lolote unalotaka kulifanya inabidi ulitathimini kwanza kabla hujalitolea maamuzi. Usifanye maamuzi wakati una haraka au una hasira. Unatakiwa kutulia na kutafakari kwanza, kwa sababu usipofanya hivyo utajikuta umetoa maamuzi ya kukuumiza na ukaishia kupata hasara.

Ukitaka Salama Ya Dunia, Zuia Ulimi Wako
Ulimi ni kiungo kidogo sana katika mwili wa binadamu lakini kimebeba mambo makubwa na mazito. Kiungo hiki kimebeba magomvi, matusi, uchochezi, utenganishi na mambo mengine mengi ambayo yanaleta vurugu katika maisha ya jamii siku hadi siku.

Anayevumilia Mpaka Mwisho Ndiye Anayekula Akashiba
Kuna jambo la kukatisha tamaa linaweza kutokea wakati imejikita na shughuli fulani halafu ukashindwa kuvumilia na pengine hata ukatangaza kuwa umechoka na wala hautaki tena kuendelea nalo. Hali hiyo ya kukata tamaa itakupelekea wewe kuacha unachofanya. Hatua hiyo siyo nzuri. Mvumilivu hula mbovu, wahenga walinena.

Ni Rahisi Kusikia Maneno ya Mdomoni Kuliko Ya Moyoni
Kilichopo ndani ya moyo wa mtu ni vigumu sana kukijua hata kama ni ndugu yako au rafiki yako. Waswahili walisema, moyo wa mtu ni msitu mnene ambao unatoa maamuzi yaliyo sahihi au magumu. Yawezekana kabisa jambo ambalo litaamuliwa na moyo likakinzana na fikra ya mtu lakini kwa sababu moyo hauna mshauri basi maamuzi yanaweza kuwa ni mabaya. Ubaya wake utaonekana baadae wakati ambao inakuwa vigumu kubadilisha.

Rafiki Wa Kwali Ni Yule Anayefahamu Matatizo Yako Na Bado Uko Naye
MAZUNGUMZO YA BUSARARAFKI WA KWELI NI YULE ANAYEFAHAMU MATATIZO YAKO NA BADO UKO NAYEALFREDA GEORGEHapa duniani tuna makundi mengi ambayo tunaishi nayo siku hadi siku. Makundi hayo yamegawanyika kutokana na hali halisi ya maisha. Kuna kundi la familia, ndugu, marafiki, na pia wale unaofanya nao kazi. Kundi hili la mwisho, kazi ndio inakuwa kiunganishi kikubwa..Kundi la marafiki huwa ni kubwa zaidi. Kundi hilo linaweza kuwa ni zuri au la kinafiki . Kuna rafiki ambaye anakuwa ni kama ndugu unaweza usimtofautishe na ndugu wa familia yako. Rafiki unaweza ukamuamini kiasi kwamba kila jambo lako utamshirikisha, liwe baya au zuri.Katika marafiki inabidi uangalie yule ambaye anaweza kubeba siri zako na kwamba kama umemshirikirsha, basi usije ukazisikia sehemu yoyote. Hapo unahitaji umakini wa kufahamu mtu aliye sahihi. Ukikosea basi utaangukia pabaya.Umakini wako utakupa rafiki mzuri na wa kweli. Rafiki huyo huwa yuko tayari kubeba matatizo yako pindi yanapotokea. Mwingine anaweza akakuacha njia panda ukihangaika peke yako. Rafiki wa aina hiyo sio rafiki mzuri .Rafiki mzuri na wa kweli, ni yule anayekufaa wakati wa shida. Ni yule anayeona tatizo lako kama la kwake the na anakuwa tayari kukutetea kwa hali na mali, kwenye jambo dogo ama kubwa, kuwe na mvua ama jua, yeye anakuwa mstari wa mbele kukusaidia wakati wowote na kwa hali yoyote, ili mradi wewe upate msaada unaouhitaji kwa wakati muafaka. Marafiki wa namna hii kwa hakika si wengi, ni wachache mno. Ukiwa nao, yakupasa umshukuru Mungu, na uwasike vizuri, usiwaachilie.

Heshima Haina Duka
Heshima ni ile hali ya kumtambua mtu katika nafasi yake. Nafasi ya mtu hutokana na vile alivyoumbwa na mara nyingi mtu anazaliwa nayo. Kama anazaliwa nayo ni ya kwake, haiwezi kuwa ya mwingine.


Zawadi Haina Udogo
Zawadi ni kitu chochote akupacho mtu bure bila kukiomba. Mtu anapokupa zawadi iwe ndogo au kubwa, unatakiwa kushukuru. Kutoa shukurani kwa vitu ama zawadi tunazopewa ni jambo la uungwana kwa mwanadamu yeyote.

Mjinga Mpe Nafasi
Tukiangalia tafsiri ya mtu mjinga tunaona kama vile ni mtu asiyefaa kwenye jamii au ndani ya familia. Mtu kama huyo hudharaulika sana hata kama akisema au akiongea kitu huwa anapuuzwa, wala hatiliwi maanani.

Uwe Mkweli Na Mwenye Maamuzi Sahihi
Kuna mambo ambayo unatakiwa kuzingatia katika maisha yako. Mojawapo ya mambo haya ni kufanya maamuzi sahihi. Ukweli unaonyesha kuwa maskini walio wengi na watu ambao wameshindwa kuendesha biashara ama waliokwama kwenda mbele, ni wale ambao wana tabia ya kushikilia mambo ya jana. Ukweli ni kwamba, jana ilikwishapita na hivyo haiwezi kukupa chochote.