Usilaumu Kimbunga, Tunza Mkeo.

Usilaumu Kimbunga, Tunza Mkeo.

Siyo jambo geni kwenye jamii zetu kusikia kuwa jukumu na wajibu wa msingi wa kila mwanaume ni kumtunza mke wake kwa kumpatia mahitaji yake ya msingi. Lakini maisha yamebadilika na hivyo kufanya majukumu yabadilike pia. Hii ni kutokana na hali ngumu ya maisha. Kwa kiasi kikubwa, wanawake wengi wamekuwa wakilalamikia wanaume kusahau majukumu yao. Hii imesababisha ndoa nyingi kuvunjika.

Read More
Usipime Mafanikio Yako Na wale Walio Kuzidi.

Usipime Mafanikio Yako Na wale Walio Kuzidi.

Mipango ya watu wengi huwa ni ya kuleta mafanikio na sio vinginevyo. Unapoweka mipango yako unaweka na mikakati ya jinsi ya kutekeleza hiyo mipango. Mikakati hiyo itatakiwa iwe na uwezeshaji, inawezekana kifedha au kimawazo. Kama ni kifedha, unaweza kutumia njia ya kukopa au vinginevyo. Kama ni kimawazo, utahitaji kupata mawazo kutoka kwa watu mbalimbali, watu wenye busara na uungwana.

Read More
Ujinga Mzigo!

Ujinga Mzigo!

Tujikumbushe kwanza hilo neno ujinga ni nini. Ujinga ni ile hali ya mtu asiyejitambua au kukosa ufahamu wa kufanya jambo lolote lenye manufaa au faida kwa kutumia akili zake mwrnyewe. Bila shaka tunajionea wenyewe jinsi Serikali yetu inavyojitahidi kutoa elimu bure kwa watoto wetu na hata kutoa mikopo kwa vijana wetu wanaoingia Chuo Kikuu. Lengo kuu la kufanya hivyo kuwapa elimu ili kufuta ujinga. Taifa linatakiwa liwe na watu wenye maarifa, uelewa na uwezo wa kujitambua wa kufanya shughuli za maendeleo ya taifa lao wakiwa na uelewa zaidi.

Read More
Kichwa Pasipo Ufahamu, Ni Mzigo Wa Shingo.

Kichwa Pasipo Ufahamu, Ni Mzigo Wa Shingo.

Tukiwa kama walezi tunatakiwa kuwa makini na ulezi tunaofanya kwenye familia zetu. Malezi yanatakiwa kuanza mapema ili kuweza kukuza familia zetu katika taratibu nzuri na salama kwa watoto wetu. Tusipokuwa makini basi watoto wetu watakua katika maisha haya tusemayo ni ya kidigitali. Tunaweza kusema kwamba tunaenda na wakati, mwisho wa siku mzigo utakuja kuwa wa kwetu.

Read More
Usisumbuke Na Wanao Sumbuka Na Wewe!

Usisumbuke Na Wanao Sumbuka Na Wewe!

Wapo watu ambao maisha yao siku zote huwa wanatafuta habari za wenzao, wao hawana lingine. Mara nyingi habari zenyewe huwa ni za kuwachafua tu wenzao. Watu kama hawa, mara zote hupenda kuwanenea wenzao mabaya Kwa malengo ya kuwafanya waonekane si kitu mbele za watu. Yote hii ni kwa sababu ya roho mbaya walizokuwa nazo, hakuna jingine zaidi. Mapenzi yao makubwa ni kuona wenzao wanaonekana vibaya mbele ya kadamnasi.

Read More
Timiza Leo Yako Ili Kuifanya Kesho Yako Iwe Bora.

Timiza Leo Yako Ili Kuifanya Kesho Yako Iwe Bora.

TIMIZA LEO YAKO ILI KUIFANYA KESHO YAKO IWE BORAALFREDA GEORGESijui wewe unatimizaje siku yako. Unaweza ukawa unalalamika kuhusu watoto wako lakini unapaswa kujiuliza wewe mwenyewe kwanza endapo umetimiza ipasavyo kwa ajili ya yale unayoyataka kwa ajili ya watoto wako.Kwa kawaida mtu huvuna alichopanda. Leo hii unapolalamika kuhusu watoto wako kutokukuelewa, ni vema ukajiuliza kwanza wewe mwenyewe, kile uluchopanda kwa ajili ya watoto wako hao. Kumbuka, ya jana huwa hayarudi.Furaha yako leo itategemea sana na maandalizi yako ya jana.Wengi tunatamani tuwe na maisha mazuri na kipato kiwe kizuri. Swali ni lile lile, kuhusu ulichopanda jana ili kuwezesha kipato chako kiwe kizuri leo.Kama unataka kesho yako iwe nzuri anza kuifanyia maandalizi leo. Kama unataka watu wakupende na upate kibali machoni pa wengi, kumbuka kupanda mazuri leo yako.Kama huoni jinsi ya kukipata unachotamani, basi amua leo kufanya vyema ili uweze kutimiza azma yako siku ya leo na uweze kuifurahia kesho yako. Maandalizi mazuri ya maisha yanatokana na jinsi ulivyojiandalia, hakuna muujiza wowote. 

Read More
Ukitaka Ubaya, Dai Chako

Ukitaka Ubaya, Dai Chako

Usemi huu unaendana na ule usemao kukopa harusi kulipa matanga. Kuna tabia ambayo imejengeka katika jamii zetu ya kusaidiana kupitia kukopeshana. Mtu anapokuwa na shida anakuja kwa machozi na heshima zote na kuweka tarehe ya kurudisha. Hata kama mkifikia kuandikishana mkataba, huwa yuko tayari. Tatizo linakuja pale muda wa kurudisha unapokuwa umepita.

Read More
Ubaya Ni Akiba Na Wema Ni Akiba!

Ubaya Ni Akiba Na Wema Ni Akiba!

Ni jambo dhahiri kuwa watu tunaishi kwa kutofautiana tabia zetu tokea utoto wetu hadi ukubwani. Jamii huwa inasoma makuzi ya familia zetu kuanzia udogoni hadi unapokuwa mtu mzima. Huchunguza matendo na maneno yatokayo midomono mwetu. Tabia ambayo unaionyesha ndicho kinakuwa kielezo tosha cha wewe kujiwekea akiba ya ubaya au akiba ya wema.

Read More
Mwenye Wivu Hashindi

Mwenye Wivu Hashindi

Hapa duniani kuna watu ambao shughuli zao kubwa ni kukatisha tamaa wenzao katika mambo mbali mbali wayafanyayo. Hiyo inatokana na roho ya wivu waliyonayo. Watu wa aina hii huwa hawawezi kumsifia mtu hata kama amefanya jambo zuri. Watu hawa huwa wako tayari kukukatisha tamaa ili ionekane ulichokifanya hakina maana yoyote ile.

Read More
Kulia Kupokezana

Kulia Kupokezana

Wako watu wenye tabia mbaya za kuchekelea au kufurahia wenzao wanapopata matatizo au changamoto katika maisha yao. Watu hawa hujisahau na hukosa ufahamu kwamba, hapa duniani, matatizo huwa ni ya mzunguko. Hii ina maana kuwa leo yakiwa kwa mwenzio kesho yatakuwa kwako, na kesho kutwa kwa mwingine.

Read More