Mafanikio Ni Mchakato!

Mafanikio Ni Mchakato!

Kwa kawaida binadamu huwezi kuhesabu mafanikio yako ukiwa umekaa au umebweteka tu. Kama ilivyo kawaida, siku huwa zinabadilika na kila siku ina mambo yake, na mafanikio vivyo hivyo. Lazima upitie mchakato ili uweze kufanikiwa. Endapo mchakato utaonyesha kukukwamishia mafanikio yako, basi elewa huo sio mchakato sahihi. Cha msingi, usikate tamaa endelea kuangalia mchakato mwingine. Unaweza hata kumshirikisha mtu ambaye unamuamini ambaye anaweza akakusaidia kwa mawazo au hata kwa mtaji.

Read More
Mpanda Hovyo Hula Hovyo.

Mpanda Hovyo Hula Hovyo.

Neno mpanda linatokana na neno kupanda. Mpanda ovyo ni yule mtu anayepanda vibaya bila mpangilio. Mtu huyu hupanda bila kufuata hatua zitakiwazo. Mathalani, wakati wa kupanda inatakiwa kuzingatia nafasi kati ya mbegu na mbegu, hali kadhalika, kati ya mstari hadi mstari. Pia inabidi kuzingatia ubora wa mbegu zenyewe ili kupata mavuno yaliyo mengi na bora. La sivyo, kinyume na hapo, mavuno yatakuwa kidogo na yenye ubora duni. Pale mavuno yanapokuwa duni hayatakidhi kuliwa kwa mwaka mzima uliotegewa. Ndio maana ya usemi huu kuwa aliyepanda ovyo, atakula kwa miezi michache tu, kinyume na mategemeo yake.

Read More
Ukiambiwa Ubaya Wa Mtu, Tafuta Uzuri Wake.

Ukiambiwa Ubaya Wa Mtu, Tafuta Uzuri Wake.

Binadamu tuna tabia moja ya ajabu sana. Mara nyingi tukiambiwa kuwa fulani ni mbaya tunaamini mia kwa mia na kuufanya ubaya wake kuwa ni fimbo ya kumchapia kila uchao. Kila jambo atakalotenda linakuwa ni baya tu kwa jamii inayomzunguka. Ubaya wake unakuwa umekwisha tia mhuri kwenye mioyo ya watu kiasi kwamba hata akipita mahali popote pale atakuwa ni wa kunyooshea vidole tu.

Read More
Donda La Kichwa Mkaguzi Mkono!

Donda La Kichwa Mkaguzi Mkono!

Ni ukweli usiopingika kuwa kila binadamu lazima atakuwa na mtu au watu wa karibu ambao huwa ni tegemeo lake katika mambo mengi ayatendayo, hususani wakati wa shida ama wakati wa raha. Wako watu ambao wanaweza kuwa karibu zaidi kiasi kwamba kunakuwa hakuna jambo unalowezakulifanya bila wao kujua au kuchangia mawazo.

Read More