Mafanikio Ya Mtu Hutegemea Uwezo Wa Kufikiri Na Kutafakari

Mafanikio ya mtu yeyote hapa duniani hutokana na bidii, kujiamini, kiwango na uwezo wake wa kufikiri na kutafakari. Aidha, wengine hupoteza muda wao kuwaza jinsi watu wengine wanavyowaona, wanavyowafikiria, wanavyowatafakari na wanayowawazia.Hata hivyo inabidi kujua kwamba, ili uweze kufanikiwa katika maisha, kamwe usitumie muda wako kuwaza kuwa nikifanya hivi wengine watanionaje ama watanifikiriaje. Inakubidi wewe ufanye shughuli zako kwa kujiamini. Ili mradi unachofanya kiwe ni sahihi mbele ya Mungu na mbele za binadamu wenzio.Kwa kuwa na mtizamo huo chanya, mawazo ya watu wengine hayataruhusiwa kuitawala akili yako. Mtazamo chanya utakufanya usimame imara kwenye kile unachokiamini na hatimaye, utapata mafanikio.Hapa tunapata funzo kuwa, kamwe tusiumize vichwa vyetu na kuchukua muda mwingi kuwafikiria watu wengine wanachowaza juu yetu. Jiulize wewe unawaza nini kuhusu wao pamoja na kwamba hata wewe siyo kazi yako kuwawazia wengine. Wewe jali kazi na maisha yako na mambo yanayokuhusu. Acha kuwafikiria wao kwani mambo yao wewe hayakuhusu.

Read More
Debe Tupu Haliachi Kutika

Debe Tupu Haliachi Kutika

Tupo katika ulimwengu wenye mambo mengi yanayotuzuguka. Kwa kawaida, maisha yetu yako katika makundi makundi. Yapo makundi yenye uwezo mkubwa, yapo yale yenye uwezo wa kati, hali kadhalika yale ya kawaida. Kundi hili la mwisho ni lile ambalo inawezekana hata riziki ya siku ni ya kubabaisha. Inaweza hata siku ikapita bila ya kuwa na chochote. 

Read More
Jifunze Kujishusha Machoni Pa Watu Wengine

Jifunze Kujishusha Machoni Pa Watu Wengine

Baadhi ya watu wana ile tabia ya kuona kwamba wao ndio pekee wa kuweza kutoa maamuzi ya aina yoyote wakiwa kwenye kundi la watu. Tabia ya watu hawa ni ya kujiona na kujisikia kuwa wao ni bora kuliko watu wengine. Watu hawa hufikia hatua ya kuchukia pale wanapotoa jambo/ushauri mbele za watu na halafu usikubaliwe. Huwa hawaelewi kabisa kwa nini yale wanayosema yasikubaliwe na watu. 

Read More
Ujana ni Dhahabu

Ujana ni Dhahabu

Katika maisha tunaweza kusema kuwa, "umri wa ujana" ni kipindi cha dhahabu ambacho tunatengeneza marafiki wengi na kupoteza wengi pia. Katika kipindi hiki, uamuzi wa kuyaharibu au kuyatengeneza maisha yako ili yawe mazuri baadaye unao wewe mwenyewe. Kwa hiyo inakupasa kukumbuka kuwa kipindi hiki kikishapita hakijirudii tena. Hivyo kitumie vizuri uwezavyo.

Read More

Usitoe Maamuzi Wakati Una Hasira

Hasira ni ile hali ya kuhamaki kwa jambo ambalo umesikia au umefanyiwa na mtu bila kukubaliana ama kuridhika nalo. Inawezekana likawa ni jambo la kusingiziwa au la. Hasira inaweza kukupelekea kuamua chochote kibaya, ukafikia hata hatua ya kuua. Mara nyingi hasira inaishia kwenye kujuta kwa lile ulilolifanya kwa kukusudia ama kutokusudia. Sambamba na usemi huu ni ule wa Majuto ni Mjukuu. Tunaaswa kutokuamua jambo lolote wakati tuna hasira.

Read More