Udhaifu Wako Usikufanye Ujiwekee Ukuta Kuzuia Mafanikio
Wakati mwingine binadamu tunakuwa na tabia ya kujidharau na kutojipenda. Huwa tunafikia hata hatua ya kujikataa na kujiona hatufai. Hali kadhalika, hujiona kuwa hatustahili kuishi na kwamba hata tukifanya kazi yoyote hatuwezi kupata mafanikio. Kuna wakati huwa tunakuwa na mtizamo hasi dhidi ya maisha yetu sisi wenyewe.
Maneno si Mkuki
Ulimi hutamka maneno yaani silabi zilizounganishwa zikaleta tamshi la kueleweka. Mkuki ni silaha ya jadi ambayo imetengenezwa kwa mti na ncha kali ya chuma. Mkuki hutumika kuwindia wanyama, hususani, wanyama wakubwa.
Heshima Hutengenezwa kwa Hekima, Haitengenezwi kwa Mkiki
Mara nyingi tunapenda kumsifia mtu tunapoona kuwa ana heshima. Lakini hatuelewi kwa nini huyo mtu yuko vile alivyo. Silaha kubwa juu ya hilo ni hekima.
Weka Bajeti Upate Mafanikio
Kuna umuhimu wa kuwa na bajeti unapoanza au unapoendesha mradi wowote. Ili uweze kuidhibiti pesa ni lazima kuwa na bajeti. Ni muhimu kuwa na bajeti kwani itakusaidia kukuonesha pesa inatoka wapi na inakwenda wapi.
Mgeni Njoo, Mwenyeji Apone
Mgeni ni mtu anayekuja kwenye makazi ambayo hana mazoea nayo au ni mahali ambapo siyo kwake. Kwa kawaida, mtu huyu anapokuja humfanya mwenyeji wake kuhangaika kutafuta hiki na kile, ili mradi yeye na mgeni wake waweze kufurahi pamoja. Mgeni huyo anaweza kuwa ni ndugu ambaye ametoka mbali kuja kusalimia tu ama kwa shughuli nyingine.
Ni Rahisi Kubeba Kikombe Kisicho na Kitu Kuliko Kile Chenye Kitu
Kwenye maisha ya binadamu, tunaposema “Ni rahisi kubeba kikombe kisicho na kitu kuliko kikombe chenye kitu“, ina maana kubwa. Kwa mfano, ukiishi na watu mbalimbali huku ukijivuna, ukiwadharau na kuwaona hawafai, hawajui kitu, ila wewe unajihesabia kuwa ndiye unayejua kila kitu, watu watakulinganisha au watakufananisha na kikombe kisicho na kitu chochote ndani yake, yaani kikombe kitupu.
Kuvunjika kwa Koleo, Sio Mwisho wa Uhunzi
Uhunzi ni shughuli za ufundi chuma. Koleo ni chombo kinachotumika na mafundi wanaojishughulisha na masuala ya chuma. Endapo katika kukata chuma kikavunjika, kitakachofanyika ni kwenda kutafuta chuma kingine ili kazi iendelee.
Achana na Neno Haiwezekani Upate Mafanikio
Ukitaka kupata mafanikio maishani mwako usiwe na mazoea ya kutumia neno ‘haiwezekani’. Mojawapo ya udhaifu mkubwa wa binadamu ni kuzoea kutamka neno hili la haiwezekani. Mara nyingi watu wenye neno haiwezekani midomomi mwao ndio ambao huwa hawafanikiwi katika maisha.
Jifunze Kutotangaza Shida Zako
Tatizo au shida humpata mwanadamu yeyote hapa duniani. Huo ndio ukweli wa maisha, kwani maisha ndivyo yalivyo. Kawaida, mtu akipata tatizo, hali yake hubadilika na tunaweza tukasema kuwa, mtu huyo huwa hayuko sawa. Anaweza akatafuta namna ya kutoka au kulitatua jambo linalomsibu. Kufanya hivyo ni hali ya kawaida sana.
Anayetembea Kwenye Matope Yampasa Asafishe Miguu Yake
Hapa duniani kuna aina nyingi za barabara. Kuna barabara zile za lami, moramu na vumbi. Ikitokea umetembea kwenye barabara ya vumbi na mvua ikawa imenyesha, utakanyaga matope.
Kuku Mgeni Hakosi Kamba Mguuni
Kuku ni ndege afugwaye kwenye makazi ya wanadamu. Kuku huchukuliwa kuwa ni kitoweo cha heshima kwa wageni wa hapo majumbani kwa watu.
Mkuki Kwa Nguruwe, Kwa Binadamu Mchungu
Mkuki ni silaha ya jadi inayotumika kuwinda wanyama wakubwa. Hapa kwenye msemo huu ina maana kuwa maneno makali ya kuumiza, kudhuru na kubomoa, kwetu sisi wanadamu inaonekana kuwa, ukimtamkia mtu mwingine unaweza kuona ni kawaida na sawa. Lakini maneno hayo hayo ukitamkiwa wewe utaona kuwa ni mabaya na utachukia kupindukia.
Kikulacho Ki Nguoni Mwako
Neno kikulacho linaelezea uharibifu ambao unaweza kutokea au kufanyika kwa makusudi au bila kukusudia ili kumuharibia mtu. Mara nyingi hilo jambo hutokea kwa watu wanaoelewana vizuri. Zaidi ni marafiki ambao huwa wanafanyiana hivyo. Hii ni kwa sababu kila mmoja anamuelewa mwenzake vizuri. Inawezekana akawa ni jirani yako au ndugu yako.
Unachokifanya Leo Kinatengeneza Kesho Yako
Jambo lolote ambalo mwanadamu analifanya linategemea sana maandalizi aliyojiwekea kwenye mipango na mikakati yake. Mafanikio hayawezi kuja kwa kufikiria tu, bali ni kwa utekelezaji wa yale uliyojipangia.
Wagombanapo Ndugu, Chukua Jembe Kalime, Wakipatana, Chukua Kapu Kavune
Ndugu ni watu waliozaliwa katika familia moja au ukoo mmoja. Ugomvi ni hali ambayo hujitokeza kwa kutokuelewana mtu na mtu. Ugomvi huu unaweza ukafikia hata kupigana.
Ulimi Ulimponza Kichwa
Ulimi ni kiungo kidogo ndani ya mwili, hukaa mdomoni na kumwezesha mtu kuongea vizuri. Kama ulimi haufanyi kazi basi mtu hawezi kuongea vizuri na mara nyingi huwa bubu.
Shida Haipigi Hodi
Shida ni tatizo au changamoto inayomfika mwanadamu. Hodi ni neno linalotumika badala ya swali la: “naweza kuingia?" Hapa anaposema shida haina hodi sio kweli maana mwanadamu anapopatwa na tatizo ataingia kwa jirani na kutoa shida zake ikibidi kuomba msaada ili atatue changamoto zake. Shida inaweza kukupeleka hata mahali ambapo hujawahi kufika.
Mbuzi Hula Kadiri Ya Urefu Wa Kamba Yake
Mbuzi ni mnyama anayefugwa kama wanyama wengine. Akipelekwa machungani huwa anafungwa kamba mguuni ili kumuwekea mipaka ya malisho yake. Mara nyingi akiachiwa huru au akikata kamba anaenda kufanya uharibifu kwa kula kwenye mashamba ya watu na mwenye mbuzi hupata kesi kubwa. Mara nyingine huweza hata kulipishwa kwa uharibifu huo uliosababishwa na mbuzi wake. Hii ndio sababu kuu ya kufungwa kwa kamba.
Upendeleo Au Ubaguzi Ndani Ya Familia Siyo Mzuri
Watoto ni zawadi kutoka kwa Mungu, hivyo tunapaswa kushukuru. Mungu anapokupa watoto wawe wa kiume, kike au mchanganyiko inabidi uridhike na kumshukuru Mungu, kwani kuna wengine ambao hawakujaliwa kupata kabisa.
Utaula Wa Chuya Kwa Uvivu Wa Kuchagua
Chuya ni mpunga ambao unakuwa umejichanganya na mchele mzuri ambao upo tayari kwa kupikwa. Hizo chuya huwa zinatakiwa kuchaguliwa ili kupata mchele mzuri, tayari kwa kupikwa. Lakini inawezekana kwa watu wengine ambao ni wavivu, kuupika mchele ukiwa hivyo haujachaguliwa wasione tofauti ama vibaya.