Mjinga Mpe Nafasi
Tukiangalia tafsiri ya mtu mjinga tunaona kama vile ni mtu asiyefaa kwenye jamii au ndani ya familia. Mtu kama huyo hudharaulika sana hata kama akisema au akiongea kitu huwa anapuuzwa, wala hatiliwi maanani.
Uwe Mkweli Na Mwenye Maamuzi Sahihi
Kuna mambo ambayo unatakiwa kuzingatia katika maisha yako. Mojawapo ya mambo haya ni kufanya maamuzi sahihi. Ukweli unaonyesha kuwa maskini walio wengi na watu ambao wameshindwa kuendesha biashara ama waliokwama kwenda mbele, ni wale ambao wana tabia ya kushikilia mambo ya jana. Ukweli ni kwamba, jana ilikwishapita na hivyo haiwezi kukupa chochote.
Unaweza Ukawa Mkwezi Na Usiweze Kusuka Pakacha
Mkwezi ni mtu ambaye huwa anaangua nazi. Pakacha ni kifaa kinachosukwa kwa kutumia makuti ya minazi ili kubebea nazi na hata vitu vingine.
Hasara Haiogopi Mtaji
Mtaji ni nyenzo ambayo inatumika kwa ajili ya kutengeneza jambo fulani lenye tija ndani yake. Inawezekana ikawa ni fedha au kitu kingine ili mradi kiweze kuleta tija. Mtaji unatakiwa uzalishe na utoe faida. Ili iweze kuwa hivyo, unahitajika umakini wa hali ya juu endapo utataka kufikia malengo uliyojipangia.
Kikulacho Ki Nguoni Mwako
Siyo watu wote hapa duniani ni marafiki wazuri. Wapo marafiki wengine ambao ni wabaya, wanafiki, wambeya, wakweli, waongo, na kadhalika.
Muongo Huwa Haulizwi
Hapa duniani kuna watu wa aina mbalimbali. Ndio maana watu husema dunia ni uwanja wa fujo. Kuna makundi mengi yenye huluka tofauti tofauti. Katika makundi hayo liko kundi moja ambalo ni gumu sana nalo ni lile kundi la waongo au wazushi. Kazi kubwa ya kundi hili huwa ni kuvuruga jamii. Watu walioko kwenye kundi hili ni wa hatari sana. Wao ni mabingwa sana wa kuleta uchonganishi na kugonganisha watu ili wasielewane. Pale wanapoona fulani na fulani wanaelewana, wao hukosa raha. Lazima watatafuta njia ama namna ya kuwavuruga. Watajitahidi kutunga uongo unaoendana na ukweli ili mradi tu waweze kuwatenganisha.
Kunguru Hashibi Jalala Moja
Maisha yana namna nyingi ya kuanza. Wapo ambao wanaanza vizuri, lakini hao ni wachache sana. Walio wengi huanza kwa ugumu, lakini baadae hufanikiwa. Kuna wale wanaoanza huku wakiishi kwa wenzao. Tunaweza tukasema hao ni tegemezi.
Hata Kobe Anafika Anakokwenda
Safari ni tendo la kutoka mahali na kuelekea mahali pengine. Inawezekana ni safari ya matembezi tu au inaweza kuwa ya kumtembelea ndugu au jamaa. Safari vilevile inaweza ikawa ni ya elimu kuelekea mafanikio. Hata kufanya biashara ni safari maana lazima uanze kidogo kidogo ndipo uweze kufikia malengo.
Mwamba Ngoma, Ngozi Huvutia Kwake
Tunazungumza kuhusu upendo kati ya mtu na mtu na ndio Muumba wetu alivyotuagiza. Mara nyingi maisha yetu yametawaliwa na ubinafsi na uchoyo. Maana hakuna mtu atakuwa na mpenyo akamkumbuka mtu wa mbali kwanza kabla ya yule wa karibu naye. Zaidi ataanza na jamaa zake wa karibu kwanza.
Mazoea Kutwaa, Kutoa Ni Vita
Kuna watu ambao wamejijengea tabia ya kupokea tu kutoka kwa wenzao, lakini wao sio wepesi wa kutoa kabisa. Watu wa namna hii, kupokea kwao huwa ni rahisi, lakini inapofika kwa wao kutoa, wanakuwa hawako tayari kabisa kufanya hivyo. Ukweli ni kwamba hata huwa hawakumbuki kurudisha fadhila walizotendewa na wengine.
Penye Mafundi Hawakosi Wanafunzi
Mahali popote penye neema hapakosi watu. Hilo ni jambo la kawaida katika familia za kiafrika. Penye mafundi ambao wana ujuzi fulani lazima pawepo na wanafunzi au watu wa kujifunza kutoka kwao. Watu husema mkulima mmoja lakini walaji ni wengi. Hayo ndiyo maisha.
Mwenda Bure Si Mkaa Bure, Huenda Akaokota
Tunaishi katika dunia ya mahangaiko ili kupata riziki ya siku hadi siku. Tunalazimika kujituma kila wakati ili kutimiza malengo yetu. Kwa hali hiyo inabidi kuzunguka zunguka hapa na pale ili kujitafutia chochote kile. Hayo ndio maisha ya mwanadamu yeyote hapa duniani.
Chanzo Cha Umasikini ni nini?
Ulegevu, uvivu na kutokuwa na bidii katika maisha ni chanzo kikuu cha umaskini. Ili ufanikiwe katika maisha inakubidi ufanye kazi kwa bidii. Usipofanya hivyo maisha yako yatakuwa hayana mwelekeo
Hasira Hasara
Mara nyingi katika maisha yetu, baadhi ya watu huwa sio wavumilivu pindi pale wnapopa taarifa mbaya. Jambo linapowafikia wanashindwa kufanya uchunguzi kwanza ili kupata ukweli. Wengi huwa wana maamuzi ya haraka, hali ambayo inaweza kuwafanya watende mambo yasiyopendeza kwenye jamii. Matokeo yake ni vurugu na magomvi na kuweka vikao vya kusutana. Hali hii huweza kusababisha watu kuwa na mahusiano mabaya na hata kununiana bila uhakika wa jambo lenyewe.
Mkono Ukupigao Ndio Ukufunzao
Kuonyana ni sehemu ya maisha. Kila mtu katika maisha yake anaweza akapata onyo, ni kawaida kabisa kwa mwanadamu yeyote. Unapopokea onyo na na kulifanyia kazi, unaweza kusonga mbele katika mambo yako uyafanyayo.
Kujifunza Ni Kila Siku
Kama unatamani kuwa vile unataka kuwa, jitahidi uvuke kawaida ya mfumo unaozaa wale wanaokuvutia.Kama unataka kuwa mtu uliyefanikiwa zaidi ya wale unaowaona wamefanikiwa, jitahidi mno uvuke kawaida, ili uende zaidi ya pale walipoishia.
Heri Kuaminiwa Kuliko Kupendwa
Siku zote, binadamu huwa tunataka kupendwa, na si vinginevyo. Huo ni ubinadamu kabisa, hakuna cha ajabu hapo. Mtu anakuwa na furaha pale anapogundua kuwa watu wanamfurahia na kumpa sifa nyingi za kumfanya aonekane ni mtu muhimu katika jamii. Lakini ni lazima tukumbuke kuwa inawezekana hao wanaokumwagia sifa wana sababu zao. Pengine ni unafiki tu na huenda kuna jambo wanalolitaka kutoka kwako. Furaha yako isiwe ya kukurupuka tu, yakupasa utafakari kwanza. Huenda mtu huyo ana jambo ambalo anataka asaidiwe katika eneo fulani linalomsumbua. Anajua kuwa ataweza kusaidiwa pale atakapokumwagia sifa lukuki.
Hakuna Anayefika Juu Kwa Kulala Usingizi
Yatupasa tujue kuwa tukipenda usingizi hatutafika popote kimaendeleo. Hiyo huwa ni dalili tosha ya kuukaribisha umaskini. Tumeshuhudia wenyewe katika maisha yetu ya kila siku. Watu wengi wenye juhudi ya kufanya kazi kwa bidii wana maisha mazuri. Wana uwezo wa kusomesha watoto wao, uwezo wa kula vizuri, hali kadhalika, uwezo wa kuwa na nyumba nzuri za kuishi.
Hatuwezi Kuibadilisha Jamii Kama Hatujabadilisha Familia Kwanza
Jamii inajumuishwa na mkusanyiko wa familia mbalimbali zinazoishi kwa pamoja kwa kufuata taratibu, sheria na kanuni za nchi. Katika hali ya kawaida tunategemea kuwa na jamii ambayo ina maadili mema ya kuweza kuliletea sifa njema Taifa letu.
Ndoa Ina Furaha, Na Maumivu Pia
Kwa kawaida kila mtu anategemea maisha ya ndoa kuwa ya furaha, lakini wakati mwingine yanaweza kuwa ni kinyume chake. Matatizo yanapoanza, matokeo makubwa ya hisia hasi, mathalani uchungu, hofu, moyo kujeruhika, wasiwasi, na hata msongo wa mawazo hujitokeza. Aidha, hisia hasi huweza kuzalisha chuki zaidi, hasira, ugomvi endelevu, usaliti, kununiana,na mawasiliano mabaya ndani ya nyumba.