Usichekelee Msiba Wa Jirani, Kelele Zitakufikia Tu.
Mara nyingi watu wanapokuwa kwenye nafasi fulani huwa wana ile hali ya kujisikia na kuona kuwa maamuzi yao ni sahihi. Hali kadhalika, huwa wanajiona kuwa wana uwezo na haki ya kunyanyasa wenzao pale wanapokuwa na uhitaji.
Cha Ndugu Hakiwezi Kua Chako, Kiogope
Watu wengi hupenda sana kujisifu kutokana na kile alicho nacho ndugu yake. Ni ukweli usiopingika kuwa mtu yeyote hatakiwi kujisifu kwa ajili ya mali ya ndugu yake. Hii ni kutokana na ukweli kuwa vitu hivyo au mali hizo siyo za kwake. Kila mtu yampasa atafute kilicho chake. Kitu kikiwa cha kwako unakuwa na uhuru nacho na unaweza ukafanya nacho chochote unachotaka.
Usimfundishe Mtu Kula Samaki, Mfundishe Kuvua Samaki
Maisha yana namna nyingi ya kuanza. Wapo ambao wanaanza vizuri, lakini hao ni wachache sana. Walio wengi huanza kwa ugumu, lakini baadae hufanikiwa. Kuna wale wanaoanza huku wakiishi kwa wenzao. Tunaweza tukasema hao ni tegemezi.
Kidole Kimoja Hakivunji Chawa
Katika maisha ushirikiano ni nguzo kubwa sana kwenye nyanja yeyote. Mahali pa kazi pakikosa ushirikiano kunaweza kutokea vurugu inayoweza kusababisha hasara kubwa. Kitakachoonekana ni mashindano ya mara kwa mara ambayo hayana tija.
Umaridadi Huficha Umaskini
Umaridadi utakuwezesha kuwa na muonekano unaotaka. Haijalishi kazi ufanyayo bali cha msingi ni kupenda kile unachofanya. Usiruhusu kazi unayofanya iwe kikwazo katika mwonekano unaotaka uwe.
Tambua Adui Anayekutafuna
Mtesi wa maisha yako ni wewe mwenyewe ndiyo maana wanasema angalia habari zako kwanza kabla ya kutafuta mambo ya wenzio. Yakupasa kufahamu kwamba unatakiwa kuyatatua yale yanayo kuhusu wewe mwenyewe kabla hujaanza kutatua ya watu wengine.
Chakula cha Mchana Hakikosi Kuni
Kuni ni nishati itokanayo na miti. Nishati hii hutumika kupikia chakula, kuchomea matofali, au kuota kwenye maeneo ya baridi kali.
Kinywa ni Jumba la Maneno
Kinywa kinahusisha mdomo na ndani yake kuna ulimi. Hapo ndipo yanapotokea maneno chanya na hasi, mazuri na mabaya. Tunasema ni jumba la maneno kwa sababu maneno yote hutokea hapo.
Bora Mchawi Kuliko Mfitini
Dunia imejaa fitina za kila aina. Wako watu ambao kazi yao kubwa ni kufitinisha au kuchonganisha watu. Mara nyingi, hali hii hutokana hasa pale wanapoona fulani anaelewana vizuri na fulani. Watatafuta kila njia ili wawakosanishe.
Chui Hakumbatiwi
Fikira za mwanadamu huwa hazina ukomo. Hii ni kutokana na ukweli kwamba binadamu ana mambo mengi ya kuwaza wakati wote. Kuna mambo tunayawaza yakiwa ni ya hatari kwetu na ya kuhuzunisha pia. Mambo ya kuhuzunisha huwezi kuyakumbatia. Mambo hayo ni kama uvivu, wizi, kutowajibika, kusengenya na kusema uongo. Ukitaka kuwa na amani, inakupasa ujitenge na mambo hayo, hii ni kwa ajili ya ustawi wako mwenyewe.
Usisamehe Kama Hauko Tayari Kusahau
Msamaha ni jambo la kiungwana ambalo mtu anafanya au anatakiwa kufanya kwa mtu ambaye amemkosea au kumuudhi katika jambo lolote. Kwa watu wengi, kuomba msamaha huwa siyo jambo rahisi, huwa kuna ugumu fulani. Ugumu huu hutokana na ile tabia ya kushindana na kujihesabia haki.
Umdhaniaye Siye
Katika maisha, wengi wetu tunaangalia sana matendo ya mwanadamu kwa juu juu, bila kutafakari kwa undani mazingira halisi au asili ya mtu huyo. Mara nyingi jambo hili linajitokeza kwa watu ambao wameishi na kuaminiana kwa vile kila jambo linaenda vizuri na pia hapajawahi kutokea kasoro yoyote kati yao.
Epuka Wasengenyaji
Wasengenyaji ni watu wasiokuwa na kazi na huwa wanawasema wenzao bila sababu ya msingi. Watu hawa ni wa hatari sana kwani huwa wanatumia muda wao mwingi katika kujadili maisha ya watu wengine. Tunashauriwa kujiepushe kujenga urafiki na watu kama hao.
Fimbo ya Mbali Haiui Nyoka
Wanadamu tumeumbwa kusaidiana. Usemi huu unatufundisha umuhimu wa kuishi vizuri na jamii inayotuzunguka. Hii ina maana kuwa ukipatwa na janga lolote, jirani yako ndiye atakuwa wa kwanza kuja kukusaidia na kukufariji. Haijalishi ni ndugu ama laa.
Tusilaumu Wala Tusihukumu Wengine
Lawama ni kitendo cha kumlaumu mtu kutokana na makosa aliyokufanyia kwa kukusudia au bila sababu. Watu wengi hawapendi kufuatilia mambo kwa kina ili kupata ukweli ambapo humfanya mtu aamini mambo bila kuchunguza. Hali hiyo husababisha wengine kuumia ndani kwa ndani bila kupewa nafasi ya kusikilizwa.
Paka Akikuambia Akulindie Samaki Wako, Usikubali
Paka ni kiumbe aina ya mnyama anayefugwa. Mara nyingi hupendelea sana kukaa jikoni.
Mwenda Pole Hajikwai
Maisha ni safari ndefu sana yenye milima na mabonde. Mara nyingi kupanda mlima huwa kuna ugumu wake na kunahitaji umakini sana ili usikwame njiani ukashindwa kufika juu kunako lengo lako.
Maisha Ni Milima Ya Kupanda Na Kushuka
Maisha ya mwanadamu yana utaratibu wake wa kupanda na kushuka. Hata ingekuwaje, hakuna mtu anayeweza kuibukia kileleni bila kwenda kwa hatua. Utaratibu uliopo ni kupanda hatua moja baada ya nyingine ndipo ufike kileleni.
Jipe Muda Wa Kufurahia Yale Uliyobarikiwa
Ni jambo la kawaida kabisa kwa binadamu kupenda kuwa na furaha siku zote za maisha yake. Lakini yatupasa tuelewe kuwa furaha hiyo haipatikani ki urahisi. Inakupasa kuhangaika na kujishugulisha ili uweze kutimiza matakwa yako na ufurahie matunda ya kazi zako. Lakini badala ya kujishughulisha, inafikia wakati tunaangalia fulani kafanya hiki au kile na ndio maana kafanikiwa zaidi. Tunafikiria kuwa mafanikio yake huenda yalipatikana kiurahisi. Hatuchukui muda kuchunguza alikotoka hadi akafikia hapo alipo. Tunafikiri yote aliyonayo aliyapata kiurahisi tu.
Mtoto Wa Mwenzio Ni Wako
Mtoto ni mwanadamu mwenye umri mdogo ambaye hajafikia kuwa mtu mzima. Kutokana na umri wa mtoto huyu kuwa mdogo, anapaswa apewe malezi bora kama vile, chakula, malazi, malezi, elimu na haki zake zote za kimsingi.