Shinda Tabia Ya Hasira Katika Maisha Yako
Hasira ni hisia za kujeruhika, zinazooneshwa na mtu baada ya kutofurahishwa na jambo alilotendewa au lililotendeka. Hasira ni hisia ambazo zinakaa ndani ya mtu.
Mafanikio Ya Ushirikiano
Ushirikiano ni mbinu ya kukuwezesha kumudu maisha mahali popote na ukiwa na mtu yeyote. Ushirikiano unahusisha pande mbili, yaani unatoa ushirikiano na unapokea ushirikiano, kwa hiyo unapojenga ushirikiano sio tu unanufaika mwenyewe peke yako, bali mnanufaika nyote , yaani pande zote mbili.
Muda Ni Mali
Matumizi ya muda wako yanaweza kukunufaisha na kukutoa hatua moja kukupeleka hatua ya juu zaidi ya maisha.Au matumizi ya muda wako pia yanaweza yakawa ni hasara kwako. Muda ni mali, tunaulinganisha na fedha.
Kichwa Pasipo Ufahamu, Ni Mzigo Wa Shingo.
Tukiwa kama walezi tunatakiwa kuwa makini na ulezi tunaofanya kwenye familia zetu. Malezi yanatakiwa kuanza mapema ili kuweza kukuza familia zetu katika taratibu nzuri na salama kwa watoto wetu. Tusipokuwa makini basi watoto wetu watakua katika maisha haya tusemayo ni ya kidigitali. Tunaweza kusema kwamba tunaenda na wakati, mwisho wa siku mzigo utakuja kuwa wa kwetu.
Usisumbuke Na Wanao Sumbuka Na Wewe!
Wapo watu ambao maisha yao siku zote huwa wanatafuta habari za wenzao, wao hawana lingine. Mara nyingi habari zenyewe huwa ni za kuwachafua tu wenzao. Watu kama hawa, mara zote hupenda kuwanenea wenzao mabaya Kwa malengo ya kuwafanya waonekane si kitu mbele za watu. Yote hii ni kwa sababu ya roho mbaya walizokuwa nazo, hakuna jingine zaidi. Mapenzi yao makubwa ni kuona wenzao wanaonekana vibaya mbele ya kadamnasi.
Taulo Sio Vazi La Kucheza Na Watoto
Kwa kadri maisha yanavyokwenda, umakini unatakiwa uzingatiwe sana. Maana jana ikipita hairudi tena. Utabaki unajutia tu jinsi wakati unavyokwenda. Utafikia mahali utajisikia vibaya kwa jinsi hali yako inavyozidi kuwa ngumu na mbaya.
Ishi Kwa Amani Na Furaha
Maisha yakikupa sababu mia moja za kutokuwa na furaha, wewe yape sababu elfu moja za kuwa na furaha.
Tatizo Huzaa Faida.
Tatizo ni tatizo, liwe la afya au la uchumi, mwisho wake litazaa faida. Hata likiwa ni tatizo la madeni, bado nalo litazaa faida. Kila tatizo lako litazaa faida katika maisha yako kwa sababu, kila tatizo lililo mbele yako, katika hali ya kawaida, utalifanyia kazi na mwisho kutakuwa na faida.
Timiza Leo Yako Ili Kuifanya Kesho Yako Iwe Bora.
TIMIZA LEO YAKO ILI KUIFANYA KESHO YAKO IWE BORAALFREDA GEORGESijui wewe unatimizaje siku yako. Unaweza ukawa unalalamika kuhusu watoto wako lakini unapaswa kujiuliza wewe mwenyewe kwanza endapo umetimiza ipasavyo kwa ajili ya yale unayoyataka kwa ajili ya watoto wako.Kwa kawaida mtu huvuna alichopanda. Leo hii unapolalamika kuhusu watoto wako kutokukuelewa, ni vema ukajiuliza kwanza wewe mwenyewe, kile uluchopanda kwa ajili ya watoto wako hao. Kumbuka, ya jana huwa hayarudi.Furaha yako leo itategemea sana na maandalizi yako ya jana.Wengi tunatamani tuwe na maisha mazuri na kipato kiwe kizuri. Swali ni lile lile, kuhusu ulichopanda jana ili kuwezesha kipato chako kiwe kizuri leo.Kama unataka kesho yako iwe nzuri anza kuifanyia maandalizi leo. Kama unataka watu wakupende na upate kibali machoni pa wengi, kumbuka kupanda mazuri leo yako.Kama huoni jinsi ya kukipata unachotamani, basi amua leo kufanya vyema ili uweze kutimiza azma yako siku ya leo na uweze kuifurahia kesho yako. Maandalizi mazuri ya maisha yanatokana na jinsi ulivyojiandalia, hakuna muujiza wowote.
Ukitaka Ubaya, Dai Chako
Usemi huu unaendana na ule usemao kukopa harusi kulipa matanga. Kuna tabia ambayo imejengeka katika jamii zetu ya kusaidiana kupitia kukopeshana. Mtu anapokuwa na shida anakuja kwa machozi na heshima zote na kuweka tarehe ya kurudisha. Hata kama mkifikia kuandikishana mkataba, huwa yuko tayari. Tatizo linakuja pale muda wa kurudisha unapokuwa umepita.
Ukitaka Kushindwa Katika Maisha, Mshirikishe Ndugu
Maisha yetu sisi binadamu yamezungukwa na mambo mengi na pia na jamii tofauti tofauti. Unaweza kuishi kwenye jamii fulani na ukaona mambo yako yanakuendea vizuri sana. Kutokana na kuwa katika hali hiyo ya kuona mambo yako yanakwenda vizuri, unaweza ukaamini kuwa uko katika usalama.
Akiba Haiozi
Akiba ni kitu chochote kinachowekwa kwa ajili ya matumizi ya baadae. Neno haiozi, lina maana ya kutoharibika au kuokufaa kwa matumizi.
Cheo Ni Dhamana
Cheo ni wadhifa ambao mtu hupewa mahali pa kazi, katika familia, au katika jamii ili kutimiza majukumu kwa lengo la kuwaletea watu wa chini yake maendeleo.
Mwacha Asili Mtumwa
Asili ya mtu yeyote ni chimbuko lake, yaani kule alikotoka. Chimbuko ama asili ya mwanadamu ni kitu muhimu sana katika maisha yake.Alikozaliwa mtu ndiko unaweza kupata taarifa zake pamoja na kumbukumbu zake zote.
Mbwa Ukimjua Jina Hakusumbui
Kwa kawaida, kila mtu anayo tabia yake ambayo mwingine hana. Huwezi ukamfananisha mtu na mtu mwingine katika nyanja yeyote ile. Binadamu tumeumbwa kila mtu kwa namna yake. Inawezekana kabisa kile unachokitaka wewe, mwingine asikipende, hivyo ndivyo maisha yanavyokwenda.
Usikatae Wito, Kataa Neno
Kuna wakati mwingine watu hufanya maamuzi ya jambo fulani bila kutafuta ukweli wa jambo hilo aliloambiwa. Inawezekana jambo aliloambiwa halina ukweli wowote ila kwa sababu ameambiwa na rafiki au jamaa yake wa karibu basi anajua hilo jambo litakuwa sahihi.
Ubaya Ni Akiba Na Wema Ni Akiba!
Ni jambo dhahiri kuwa watu tunaishi kwa kutofautiana tabia zetu tokea utoto wetu hadi ukubwani. Jamii huwa inasoma makuzi ya familia zetu kuanzia udogoni hadi unapokuwa mtu mzima. Huchunguza matendo na maneno yatokayo midomono mwetu. Tabia ambayo unaionyesha ndicho kinakuwa kielezo tosha cha wewe kujiwekea akiba ya ubaya au akiba ya wema.
Ishi Kwa Viwango Ulivyojaliwa
Katika maisha ya mwanadamu hapa duniani, Mungu amemjalia kila mtu karama na vipawa kwa biwango anavyostahili. Kutoka Hali hiyo, tunashuhudia kwenye jamii zetu kila mtu anafanya vitu tofauti na mwingine, pengine vinaweza vikafanana kwa kiwango kidogo tu.
Mwenye Wivu Hashindi
Hapa duniani kuna watu ambao shughuli zao kubwa ni kukatisha tamaa wenzao katika mambo mbali mbali wayafanyayo. Hiyo inatokana na roho ya wivu waliyonayo. Watu wa aina hii huwa hawawezi kumsifia mtu hata kama amefanya jambo zuri. Watu hawa huwa wako tayari kukukatisha tamaa ili ionekane ulichokifanya hakina maana yoyote ile.
Kulia Kupokezana
Wako watu wenye tabia mbaya za kuchekelea au kufurahia wenzao wanapopata matatizo au changamoto katika maisha yao. Watu hawa hujisahau na hukosa ufahamu kwamba, hapa duniani, matatizo huwa ni ya mzunguko. Hii ina maana kuwa leo yakiwa kwa mwenzio kesho yatakuwa kwako, na kesho kutwa kwa mwingine.