Wema Sio Deni, Usisubiri Kulipwa.
Kuna tabia iliyojengeka katika jamii ya kufikiria kuwa unayemfanyia wema ni lazima akulipe. Kuna wale ambao wamesomesha watoto, ndugu na jamaa wengi tu kwa kutegemea kuwa watarudishiwa fadhila kwa wema walioufanya. Kwa bahati mbaya, watu hawa hungojea weee na kukuta hakuna majibu wala fadhila yoyote inayokuja. Hizo huwa ni hisia au mategemeo ya walio wengi.
Mtaka Cha Uvunguni, Shart Ainame!
Hakuna mafanikio yatakayokujia ukiwa umekaa tu ma kubweteka huku ulingojea msaada kutoka kwa ndugu, jamaa na marafik. Mafanikio yanahitaji kujishughulisha ili uweze kuhimili changamoto zinazojitokeza. Maana kila unachokifikiria lazima kitakuwa na pingamizi au maswali ambayo ni hasi na magumu.
Tabia Zako Zinaweza Kukufanya Upoteze Fedha Zako!
Tabia zako zinaweza kukufanya upoteze fedha zako, ziwe nyingi au chache.
Ujuzi Hauzeeki!
Ujuzi ni ufundi au kipaji cha kufanya vitu ili kukuletea faida au kukuingizia kipato. Ujuzi unaweza kupatikana kupitia mafunzo. Hali kadhalika, ujuzi unaweza kutokana na kipaji cha kuzaliwa nacho mtu ambacho kinamuwezesha kufanya vitu vya pekee na vizuri vinavyoweza kununuliwa na watu na hivyo kukupatia kipato.
Mlibua Nchi Ni Mwananchi.
Mlimbua nchi ni mtu ambaye anaifahamu sana nchi yake. Kwamaneno ya sasa huyu mlimbua nchi tunasema mhujumu wa nchi yaani anaisema vibaya nchi yake; anatoa siri za nchi yake, anaiweka nchi yake katika hali ya hatari kwa namna yeyote anayotaka yeye.
Haki Ya Mtu Hailiki!
Haki ni kitu halali kinyume cha batili. Mwenye kutoa haki ni Mwenyezi Mungu peke yake, Yeye akisema amesema huwa hakuna wa kumpinga. Mwenyezi Mungu anaweza kuwatumia watu wakupatie haki yako. Mara nyingi tunaona na kuthibitisha ukweli wa usemi huu wa haki ya mtu hailiki bali hucheleweshwa tu.
Unaeokota Naye Kuni Ndiye Unaeota Naye Moto.
Kuni ni mojawapo ya nishati inayotumika sana barani Afrika. Kwa kawaida, kuni zinaokotwa au kukusanywa kutoka kwenye miti porini.
Kipimo Chako Siku Zote Ni Ufanisi.
Binadamu wote tumeumbwa tofauti katika nyanja nyingi. Wengi huwa wana ile hali ya kutaka kueleweka au kutambulika hata kama hawana jambo la maana walifanyalo. Kama ule usemi wa debe tupu haliachi kutika ndivyo ilivyo kwa wengi katika jamii zetu.
Mafanikio Ni Mchakato!
Kwa kawaida binadamu huwezi kuhesabu mafanikio yako ukiwa umekaa au umebweteka tu. Kama ilivyo kawaida, siku huwa zinabadilika na kila siku ina mambo yake, na mafanikio vivyo hivyo. Lazima upitie mchakato ili uweze kufanikiwa. Endapo mchakato utaonyesha kukukwamishia mafanikio yako, basi elewa huo sio mchakato sahihi. Cha msingi, usikate tamaa endelea kuangalia mchakato mwingine. Unaweza hata kumshirikisha mtu ambaye unamuamini ambaye anaweza akakusaidia kwa mawazo au hata kwa mtaji.
Maji Hayasahau Ubaridi.
Kwa kawaida maji huchemshwa ili yawe ya moto. Lakini taratibu maji hayo hupoa na kurudi kwenye uhalisia wake. Vivyo hivyo, tabia ya mwanadamu huwa haiwezi kujificha kwa muda mrefu bila kurudi kwenye uhalisia wake.
Zuia Mawazo Hasi.
Upo ule wakati kwenye maisha yako unaona kama umefika mwisho kabisa.Yaani, kila ukijiangalia unaona kabisa hauna nguvu tena za kuendelea mbele.
Jitie Moyo Kila Wakati!
Haijalishi unapitia changamoto gani kwenye maisha yako, jitahidi kupata muda wa kujipa moyo. Kama ni chakula kula vizuri mlo kamili ili usiidhuru afya yako halafu ukasababisha magonjwa sugu.Pia pata muda wa kujijali yaani jipendezeshe kuoga na upake mafuta yako ung'are na uvae vizuri.
Usifanye Maamuzi Kwa Ajili Ya Leo Tu, Angalia Na Kesho Yako.
Usibamize mlango wakati wa kuondoka. Ukifunguliwa na mtu /watu mlango uliouhitaji siku ukitaka kuondoka usiubamize huo mlango kwa nguvu , huenda kesho ukahitaji kuutumia tena wakati wa kuingia.
Elewa Kusudi La Kuwepo Kwako!
Uwepo wa kila mtu unakuwepo tokea mtu akiwa tumboni mwa mama yake. Hivyo ulivyo sasa ni kusudi ambalo ulizaliwa nalo. Kutokana na hali hiyo unatakiwa kujua kusudi lako ili uweze kupanga namna ya kupata mafanikio.
Kaa Mbali Na Wenye Fikra Hasi, Kwao Hakuna Jema!
Watu wenye fikra hasi ni wale wanaopenda kukatisha tamaa wenzao kwa kila wanalolitenda. Wao kazi yao ni kukandamiza tu wenzao na pia ni kujaribu kwa kila hali kufuta maono ama ndoto za wenzao.
Huwezi Kupata Kivuli Kwenye Mti Uliopinda!
Mti ni nishati ambayo ina matumizi mengi sana. Kwenye mti tunapata matunda, tunapata mbao, kuni na hata dawa. Wengine hupanda miti kwa ajili ya kivuli, hususan kwenye maeneo ya kuzunguka makazi yao.
Usitengeneze Kundi La Kumchukia Mtu Kwa Chuki Zako Binafsi!
Ulimwengu huu umejaa shida na vurugu tele kila uchwao. Karibia kila siku tunakutana na mambo mengi mazuri na mabaya pia. Mambo yaliyomabaya hutokana na mahusiano katika jamii nyingi. Migongano ya mtu na mtu au kikundi na kikundi, ni mambo ya kawaida katika maisha tunayoyapitia.
Mtenda Wema Ana Malipo!
Hapa duniani yako mambo mengi sana tusiyoyajua. Lakini ili tufanikiwe katika jambo fulani lazima tuwe na ufahamu na hilo jambo.
Usihukumu Kitabu Kwa Ganda La Juu.
Katika maisha yetu sisi binadamu tuna mambo ya kudharauliana sana. Hiyo inakuja kwa sababu ya kutokumuelewa mtu kwa undani wake. Inatokea pengine mtu kwa kukuangalia tu anakutafsiri kwa jinsi anavyokudhania yeye.
Uvivu Ni Adui Wa Mafanikio
Uvivu ni kizuizi kikuu cha mafanikio yabinadamu yeyote. Hata maandiko matakatifu yanadhihirisha hayo kwa kusema kuwa mvivu siku zote hufa maskini na hatakiwi kupewa chakula. Tunaambiwa kuwa mwenye bidii hula jasho lake ambalo ni bidii yake mwenyewe na hufa akiwa tajiri.