Omba Ufahamu Katika Maisha Yako!

OMBA UFAHAMU KATIKA MAISHA YAKOALFREDA GEORGEUfahamu ni kujua kipi ni kizuri kwako na kipi ni kizuri kwa jamii inayokuzunguka.Hali kadhalika, ufahamu ni kujua kipi ni kibaya kwako na kipi ni kibaya kwa binadamu wenzio ili uweze kukiepuka.Mtu yeyote mwenye ufahamu hutembea katika haki. Hata kama kuna jambo baya, atalihukumu katika haki.Katika maisha, inakupasa ujihukumu mwenyewe kwanza pale unapokuwa umekosea. Usisubiri watu wakuhukumu. Watu wengi wana tabia ya kupenda kuhukumu wenzao na sio kujihukumu wenyewe. Hapo ndipo vurugu na kutokuelewana kunapoanzia. Ni kawaida ya wanadamu kupenda kujitetea kwanza. Ukijua kujihukumu katika yale mabaya unayoyatenda, basi utabadilika. Utakuwa mtu wa kuheshimu kila apitae mbele yako.Usipoweza kujihukumu mwenyewe hautakaa ubadilike, zaidi utawachukia wale ambao wanataka ubadilike. Ukweli ni kwamba, ukiwa na tabia hiyo, hautaishia popote zaidi ya kushindwa.Hatua ya kupata ufahamu, huwa ni ngumu sana kuifikia. Hii ni kutokana na ukweli kwamba kuna vikwazo vingi vya kukutoa katika ufahamu. Hapo ndipo panahitaji uvumilivu maana mambo mengine yatakuudhi na kukukatisha tamaa.Ukibahatika kupata ufahamu, utakuwa umepata kila unachohitaji katika maisha yako. Kwa kawaida, Mungu humtumia mtu mwenye ufahamu na huyo ndiye atakaye sababisha upate kile ambacho umekuwa ukikitamani siku zote. Ili uwe na maisha mazuri, yakupasa uombe kutunukiwa ufahamu na hapo ndipo utakapopata amani.

Read More
Pakacha Kulivunja Nafuu Ya Mchukuzi!
Swahili Wisdom Swahili Wisdom

Pakacha Kulivunja Nafuu Ya Mchukuzi!

Pakacha ni aina ya kapu litumikalo kubebea vitu. Mchukuzi wa kapu hili ni mtu anayebeba mizigo, aidha ikiwa ndani ya pakacha au chombo kingine. Pakacha likijaa vitu linaweza likawa zito lakini jinsi lilivyosukwa linaweza kuruhusu vitu vilivyowekwa humo ndani kuvuja au kumwagika kidogo kidogo wakati vimebebwa na hivyo kupungua kwa uzito ambao humpa ahueni mbebaji /mchukuzi.

Read More
Bora Lawama Kuliko Fedheha!
Wisdom Wisdom

Bora Lawama Kuliko Fedheha!

Lawama ni ile hali ya mtu kulalamikiwa ama kushutumiwa kwa kukosa ushirikiano au kupuuza mambo angamizi kwenye jamii. Na fedheha ni ile hali ya kudhalilika au kuaibika kutokana na kutenda jambo lisilokubalika kwenye jamii.

Read More
Jembe Halimtupi Mkulima!

Jembe Halimtupi Mkulima!

Jembe ni nyenzo inayotumika na mkulima wakati wa kilimo. Kuna majembe ya aina mbalimbali, mfano, jembe la mkono, jembe la kukokotwa na ng'ombe. Hali kadhalika, kuna majembe ya kufungwa na kukokotwa na trekta. Hii yote ni kumwezesha mkulima alime na kupata mazao ya kuridhisha ili aweze kujikimu.

Read More
Mwembe Wa Uwani Nyani Hatambi!

Mwembe Wa Uwani Nyani Hatambi!

Ni kawaida kwa jamii nyingi kupanda miti ya matunda uwani kwa nyumba zao. Miti ya matunda hii ni kama miparachichi, miembe, mikomamanga na kadhalika. Kwa kufanya hivyo, watu hawa wanakuwa na uhakika wa kupata mavuno na kuyafaidi kwa sababu ndege pamoja na wanyama waharibifu, kama nyani, ngedere nk hawawezi kutamba hapo kutokana na ukweli kwamba wakati wote kunakuwepo na watu. Endapo wanyama hao watakuja, lazima watafukuzwa na wenye matunda.

Read More
Angalia Namna Ya Kuongea Kwako.

Angalia Namna Ya Kuongea Kwako.

Lugha inaweza kubadilisha hali ya hewa katika mambo mengi ufanyayo. Matumizi ya lugha yanaweza kubadilisha maisha yako na jamii inayokuzunguka. Maisha ya ndoa yako, kama wewe ni mwanandoa, yanaweza kubadilika pia. Malezi ya watoto yanaweza yakabadilika katika familia zetu kutokana na luga tunazotumia. Lugha kali kwa watoto huwaogopesha kiasi hata kukosa amani na wazazi. Watoto wakiishi kwa woga, wanaweza hata kuingia kwenye makundi mabaya ili kupata faraja. Nyumbani watapaogopa, hawatapenda kukaa na hasa pale mzazi mwenye lugha ya kukera akiwepo. Watoto wakiishi katika mazingira hayo, wanaweza kujifunza mambo yasiyofaa. Wahenga walisema, samaki mkunje angali mbichi, akikauka hakunjiki.

Read More